Tanzania na Indonesia zimekubaliana kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Nchi hizo kwa kukuza ushirikiano katika Sekta za Uchumi wa Bbuluu, Kilimo, Madini, Afya Diplomasia Biashara na uwekezaji.
Katika ziara ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Ttanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Nchini Indonesia ambapo Viongozi hao wanashuhudia mabadilishano ya hati 4 za makabaliano na barua moja ya kusudio kati ya Nchi hizo.
Akizungumza katika Ikulu ya Bogor Mjini Jarkata katika ziara yake ya kitaifa Nchini Indonesia Rais Dkt .Samia amesema makubaliano hayo yataimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi ambayo yanatimiza miaka 60.
Ameyataja maeneo waliyokubaliana kushirikiana kuwa ni pamoja na biashara na uwekezaji katika Sekta ya Mafuta na Gesi, Sekta ya Kilimo katika nyanja ya mbolea, Sekta ya Madini, na Elimu ya juu.
Raisi wa Indonesia Mhe, Joko Widodo amesema uhusiano kati ya Mataifa haya umezidi kuimarika na kuongeza kuwa Nchi yake ipo tayari kuisaidia Tanzania katika Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya.
Mapema baada ya kuwasili Raisi Dkt.Samia alipokelewa na mwenyeji wake Raisi wa Indonesia Joko Widodo na kupigiwa mizinga 21 na kupanda mti wa kumbukumbu ikiwa ni ishara ya utunzaji wa mazingira na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.