Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA-Zanzibar) kimesema ni wajibu kwa Wanawake kushiriki Michezo kutokana na kuimarisha Afya zao na kupata fursa ya Ajira.
Akizungumza katika madhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Mkurugenzi wa Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA-Zanzibar) Dkt. Mzuri Issa amesema asilimia kubwa ya Wanawake bado wako nyuma katika kushiriki Michezo jambo ambalo limesababisha kuwa nyuma kimaendeleo na kushindwa kufikia ndoto zao.
Meneja Idara Mitaala na Vifaa kutoka Taasisi ya Elimu Zanzibar Wanu Ali Makame amesema Maadhimiso hayo ni pamoja na kuunga mkono juhudi za Watoto wa Bara la Afrika kwa kupigania haki za Watoto Wenzao.
Mshauri wa Michezo wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Ujerumani GIZ, hHija Mohammed Ramadhan amesema katika Mradi wa Wanawake na Maendeleo itasaidia kuimarisha Afya za Watoto, kuondosha unyanyasaji wa kijinsia kwa Watoto pamoja na kuimarisha usawa wa Kijinsia
Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na TAMWA Zanzibar kwa kushirikiana na Idara ya Michezo, Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Taasisi ya Maendeleo ya mashirikiano ya Ujerumani (GIZ) na Kituo cha Mijadala kwa Vijana (CYD), yalitanguliwa na Mashindano ya riadha yaliyoanzia Forodhani hadi Mnazi Mmoja na washindi kutunukiwa Nishani za Dhahabu, Fedha na Fedha taslimu.