Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka Taasisi ya Big Philanthropy ya Uingereza kushirikiana na Serikali kwa mpango wa lishe Skuli katika kupunguza Utoro na kuongeza Ufaulu.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Big Win Philanthropy, Dkt. Kesete Admasu na Ujumbe wake waliofika Ikulu Jijini Zanzibar.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Admasu ameeleza kuwa wako tayari kushirikiana na Serikali katika fursa za kuwajengea uwezo watendaji wa Serikali pamoja na ushirikiano wa Sekta mbalimbali za Umma.
stories
standard