SMZ KUCHUKUA HATUA WANAOHARIBU MIKARAFUU

WILAYA YA KATI

     Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema itawachukulia hatua za kisheria Wananchi watakaobainika kuharibu au kukata Mikarafuu kinyume na sheria. 

      Akizungumza na Wakulima na Wadau wa Karafuu kutathmini Msimu wa Karafuu uliopita huko Dunga Mkuu wa Wilaya ya Kati Sadifa Juma Khamis amesema vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya Wananchi vinaitia hasara Serikali.

    Amesema Serikali ya Wilaya itashirikiana na Shirika la Biashara Zanzibar ZSTC kuimarisha Zao la Karafuu kwa kuwasimamia Wakulima kuendeleza Zao hilo lilete tija kwao na Taifa.

    Nae Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC Ndg.Soud Said Ali amesema Shirika linaendelea na Mikakati ya kuimarisha Zao hilo ikiwemo kueweka Mizani za Kisasa na Mashine za kupimia viwango vya Karafuu. 

    Wakulima wa Zao la Karafuu wamesema bado wanakabiliwa na Tatizo la Vifo vya Mikarafuu, utiaji wa Wanyama Shambani na ucheleweshaji wa Ugawaji wa Miche ya Mikarafuu 

   Aidha wameliomba Shirika la ZSTC kuwapatia elimu mara kwa mara ya uzalishaji wa Mikarafuu ili kuzalisha Karafuu bora na zenye tija

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.