Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali inatarajia kupata wastani wa Shilingi Trilioni 2 nukta 4 kutokana na Biashara ya Kaboni ambazo zitachangia kuimarisha pato la Taifa.
Dkt. Jafo ameliarifu Bunge wakati akijibu swali la Mbunge wa Buhigwe Mhe. Kavejuru Felix aliyetaka kujua biashara ya Kaboni katika misitu ya asili na ya kupanda imechangia kiasi gani kwenye pato la Taifa tangu iingie Nchini.
Aidha Waziri Jafo amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea kutoa Elimu kwa Wananchi na kuwahamasisha kupanda Miti kwa wingi ili kunufaika na Biashara hiyo.
stories
standard