Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza kujenga ukuta katika eneo la Nungwi Zanzibar kwa ajili ya kuzuia maji ya Bahari kuingia kwenye makazi ya Wananchi kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ameyasema hayo wakati akijibu maswali Bungeni Jijini Dodoma.
Katika hatua nyingine Mhe.Khamis ametoa rai kwa Wananchi kuacha kufanya shughuli zinazoharibu mazingira ya Visiwa.
stories
standard