Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dr Khalid Salum Mohammed amesema Serikali zote mbili zinaunga Mkono juhudi za Sekta Binabsi kwa kuendana na Sera za Serikali katika kufikia mabadiliko ya Kidigitali.
Akizungumza katika Hafla ya Uzinduzi wa ushirikiano wa Kidigitali baina ya Kampuni ya simu ya Airtel Money na Zanzibar Cable Televition Dr Khalid amesema juhudi za Sekta Binabsi zinaakisi vipaumbele vya Serikali ikiwemo Uchumi wa Blue Utalii na uunganishaji wa Miundombinu ambayo vinategemea mabadiliko ya Kidigitali ili kufikia maendeleo endelevu.
Mkurugenzi Airtel Money Andrew Rugwamba amesema wanarahisisha huduma kwa Wateja pamoja na kukuza uchumi na Biashara ili kuhakikisha mpango huo unafikiwa.
Mariam Mwamnyalla Meneja huduma za Airtel Money amesema wanatoa huduma za Kifedha katika Nchi 14 na Mawakala 220 kwa Nchi nzima kwa kutumia njia ya Teknologia ya kisasa.
Kaimu Mkurugenzi Zanzibar Cable Hafidh Kassim amesema wanatoa huduma kwa njia ya Air tel Money katika maeneo ya Zanzibar kwa ushirikiano mzuri na Kampuni yenye ubia kwa Serikali na Airtel Money na Zanzibar cable.