Bodi ya Sukari Nchini imesema itachukua hatua kali ikiwemo kufuta Leseni kwa Mawakala na Wafanyabiashara watakaoshindwa kuzingatia Bei elekezi iliyotolewa na Serikali kwa Bidhaa hiyo.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar Es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari, Profesa Kenneth Bengesi wakati wa zoezi la kupakia Sukari kwenye Bandari kavu ambayo inapelekwa Mikoani ili kukabiliana na uhaba wa Bidhaa hiyo.
Profesa Bengesi amesema ni muhimu Wafanyabiashara kufuata Bei elekezi iliyopangwa ambayo ni kati ya 2700 mpaka 3000 kwa sababu Serikali imeamua kufuta Kodi na Tozo zilizopo kwenye Bidhaa hiyo ili iingie kwa wingi hapa Nchini.
Kwa upande wake Fimbo Butallah ambae ni Mkurugenzi wa Biashara Kilombero, amesema matokeo ya Sukari hiyo kuingia Nchini ni baada ya Serikali kutoa Vibali cha kuruhusu Sukari kutoka Nje ya Nchi kuingia Nchini.