Serikali inatarajia Kutunga Kanuni Mpya za Utoaji Leseni za Uchimbaji wa Madini Nchini kuanzia Mwezi Julai Mwaka huu ili kuwadhibiti baadhi ya Watu wenye tabia ya kumiliki Leseni za Uchimbaji bila ya kuchimba na badala yake huzikodishwa kwa Wengine.
Hali hiyo imeelezwa na Waziri wa Madini Nchini, Anthony Mavunde kwenye Mkutano wake na Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu katika Eneo la Ntambalale Kata ya Segese Wilaya Kahama Mkoani Shinyanga.
Ofisa Madini Mkoa wa Kimadini Kahama, Joseph Kumburu alizungumzia changamoto ya Mikataba kwa Wachimbaji huku Mmoja wa Wachimbaji Wadogo alitoa Kilio chake mbele ya Waziri.
stories
standard