Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuchukua juhudi katika kuimarisha Sekta ya Kilimo ili iweze kumsaidia Mkulima katika uzalishaji na upatikanaji wa uhakika wa Chakula Nchini na kuwa Endelevu.
Waziri wa Kilimo umwagiliaji Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis ameeleza hayo huko katika Bonde la Mpunga Kilombero wakati wa zoezi la Uzinduzi wa uvunaji wa Mpunga kwa Wakulima na Maafisa wa Kilimo.
Amesema juhudi hizo zinaenda sambamba katika kuwainua Wakulima hasa katika kuwajengea Miundombinu imara katika shughuli za Kilimo ili zitumike katika kuleta maendeleo makubwa na kujipatia Kipato.
Mratibu wa Bonde hilo Yussuf Faki Yussuf wamemuomba Waziri huyo kuwasaidia katika punguzo la Bei ya pembejeo, punguzo la Umeme na kuzungumza na Watu wa Benk ili waweze kua karibu yao katika kuwapatia Mikopo ili waweze kuendelea na shughuli zao za Kilimo.
Mkulima wa Bonde hilo akizungumza kwa Niaba ya Wakulima wenziwe sijawa Hamdu Makame wametoa Shukran zao za dhati kwa Waziri huyo kwa ujio wake wa kushirikiana na Wakulima katika uzinduzi huo.
Bonde la Mpunga la Kilombero la Zone ya pita utazame B lina jumla ya heka 40.75 na Lina Robo 163 ambazo Wakulima waliopo hapo ni 158 wakiwemo Wanawake 62 na Wanaume 96