Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe. Ali Suleiman Ameir na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Yusuf Makamba wamesema kwa misingi ya Utawala bora Serikali inapotaka kutunga Sera lazima ipate maoni ili Sera inayotungwa iwe bora na izingatie maoni ya Wananchi na Wadau.
Wakizungumza katika Kongamano la tatu la kukusanya maoni ya Wadau Mahsusi kuhusu marekebisho ya Sera mpya ya mambo ya Nje ya Mwaka 2001 huku Uwanja wa Ndege Mawaziri hao wamesema kazi ya kutoa maoni juu ya Sera hiyo ni muhimu kutokana na kuwa nyenzo katika kujenga maslahi mapana ya Taifa na kukuza uchumi na maendeleo ya Taifa.
Wamesema kutokakana na mabadiliko ya Dunia ni lazima Sera hiyo kufanyiwa marekebisho ili kwenda sambamba na Sayansi na Teknologia ya sasa.
Wakitoa maoni washiriki wa Kongamano hilo wameomba masuali muhimu yazingatiwe ikiwemo Wanawake kupewa nafasi ya Ubalozi kwa kuzingatiwa vigezo, suali la Uchumi wa Buluu pamoja na Vijana katika kufikia Maendeleo.
Mada mbali mbali zimewasilishwa katika Kongamano hilo ikiwemo Sera ya mambo ya Nje hali ilivyo sasa na mambo mengine yanayohusiana na hayo, dhana ya Uchumi wa Buluu kwa kuzingatiwa masuali mapya yanayopendekezwa.