SERIKALI ITAENDELEA KUTOA KIPAUMBELE KWA WATU WENYE ULEMAVU KWA KUWAWEKEA MAZINGIRA RAFIKI YA KIJIFUNZA

MAKAMO WA PILI WA RAISI

Serikali itaendelea kutoa kipaumbele kwa Watu wenye Ulemavu  kwa kuwawekea mazingira rafiki ya kijifunza na kuhakikisha kuwa kundi hilo haliachwi nyuma katika mipango ya Serikali.

Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwa katika muendelezo wa shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi,amezunguza na Wananchi wa Pujini Wilaya ya ChakeChake katika ufunguzi wa kituo cha elimu mjumuisho, ambapo amesema Zanzibar inatekeleza mipango ya Kitaifa na Kimataifa kuhakikisha Skuli na Majengo yote yanazingatia mahitaji ya watu wenye Ulemavu.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe Lela Mohamed Mussa amesema uzinduzi wa kituo hiicho unatokana na ongezeko la Wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambao walikuwa wakikosa Skuli zinazoendana na mahitaji yao.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khamis Abdulla Said amesema inatekeleza Sera na ilani ya uchaguzi kuhakikisha makundi yote yanapata haki stahiki kwa usawa.

Kituo hivho chenye Majengo saba ikiwemo dakhalia umetumia zaidi ya Shilingi  Bilioni 4.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.