SERIKALI ITAENDELEA KUTHAMINI MCHANGO WA WASANII WAKONGWE NCHINI

WASANII WA WAKONGWE

    Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Baraza la Sanaa Sensa, Filamu na Utamaduni Zanzibar imesema bado inathamini mchango mkubwa unaotolewa na Wasanii katika kuhakikisha Sanaa inaimarika Nchini.

   Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Idara ya Utamaduni Zanzibar Dkt.Omar Salum Muhammed baada ya Ziara yakuwatembelea baadhi ya Wasanii Wakongwe walioitumikia saana hapa Zanzibar , ambapo amesema niwajibu wao kama Idara kupitia Wizara kuandaa Ziara ya kuwatembelea Wasanii Wakongwe ili kujuwa afya zao pamoja kuthamini jitihada zao.

   Mrajisi wa Baraza la Sanaa, Sensa,   Filamu na Utamaduni Zanizibar, Abdillah Ramadhan amesema lengo la kuwatembele

Wasanii hao nikuhakikisha kwamba Wasanii Chipukizi wanashajihika kupitia Vipaji vyao pamoja na kuunga Mkono jitihada za Mheshimiwa Rais wa Zanzibar.

   Baadhi ya Wasanii Waliotembewa katika Ziara hiyo wameishukuru Idara ya Utamaduni kwa kuthamini juhudi mbalimbali za Wasanii hao.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.