RAIS WA ZANZIBAR DKT HUSSEIN ALI MWINYI ANAONGOZA KWA KUFUATA SHERIA NA KATIBA YA NCHI.

MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Charles Hilary amesema ,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi anaongoza kwa kufuata Sheria na katiba ya Nchi.

Akitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari juu ya maoni yanayopendekeza kwa Dkt Mwinyi kuongezewa muda wa kubaki Madarakani kwa Miaka Saba Badala ya Mitano iliyoanishwa katika Katiba ya Zanzibar amesea maoni yaliyotolewa si ya Rais wala Chama cha Mapinduzi huku akisisitiza kuwa Dk Mwinyi ataendelea kuheshimu utaratibu uliowekwa wa Rais kuchaguliwa kila baada ya Miaka Mitano.

Hivyo amewataka wote wenye mawazo tofauti na hayo kuacha Mjadala huo kwani jambo hilo halina tija na faida kwa Nchi na Chama cha Mapinduzi chenye kufuata misingi ya Demokrasi.

Wakati huo huo Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na dk Hussein Mwinyi ameongoza kikao cha kawaida cha Kamati maalum ya Halmashauri ya CCM Zanzibar katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.