Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan,amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua za kuimarisha utendaji kazi wa Mahakama ikiwemo matumizi ya Tehama na pia amewataka Majaji na Mahakimu kuishi katika misingi ya Viapo vyao kwa kutenda haki.
Rais Samia ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya sheria Nchini inayobebwa na kaulimbiu isemayo Umuhimu wa Dhana ya Haki Kwa Ustawi wa Taifa na nafasi ya Mahakama na Wadau Katika Kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki.
Aidha Rais Samia ameitaka Mahakama kuona umuhimu wa kuimarisha haki madai kutokana na kuwepo kwa malalamiko toka kwa Wananchi na kupelekea kucheleweshwa kwa kesi
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Khamis Juma amesema kuwa mwelekeo wa utoaji wa haki Nchini unaenda sambamba na matumizi ya mifumo ya Tehama