WANANCHI WILAYA YA KUSINI KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA

ZEC

Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Kamishna Ayoub Bakari Hamad amewataka Wananchi wa Wilaya ya Kusini kuendelea kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Wapiga kura linaloendelea katika wilaya hiyo

Akizungumza baada ya kukagua Vituo vya uandikishaji Wapiga Kura wapya katika Wilaya ya Kusini amesema hatua hiyo itawawezesha kutumia haki yao ya Democrasia ikiwemo kupiga kura katika uchaguzi mkuu. 

Afisa uandikishaji Wilaya ya Kusini Samson Ezekel Kibona amesema kazi hiyo inaendelea vizuri ambapo Jumla ya Vituo 21 vimetumika kuandikisha Wapiga kura wapya.

Kazi hiyo ya uwandishaji wa Wapiga kura wapya inatarajiwa kuendelea January 13 kwa Wilaya ya Mjini.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.