Dkt Samia Ameyasema Hayo Huko Madungu Katika Hafla Ya Ufunguzi Wa Jengo La Uwekezaji La Shirika La ZSTC Ikiwa Ni Katika Shamra Shamra Za Miaka 6o Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Na Kusema Hatua Hiyo Itasaidia Kuzalisha Karafuu Kwa Kiwango Kikubwa Ili Kukidhi Mahitaji Ya Soko La Dunia.
Amesema Amefurahishwa Na Hatua Iliyofikiwa Na ZSTC Kwa Ununuzi Wa Vifaa Vinavyokwenda Na Wakati Uliopo Jambo Jambo Litasaidia Katika Upatikananji Wa Soko La Uhakika La Karafuu.
Mapema Waziri Wa Biashara Na Maendeleo Ya Viwanda Mh Omar Saidi Shaaban Amesema Shirika Kwa Sasa Limefanya Mageuzi Makubwa Katika Ununuzi Wa Karafuu ,Huku Wakiendelea Kudhibiti Magendo Ya Karafuu Kwa Kuongeza Bei Ya Zao Hilo.
Akitoa Maelezo Kwa Rais Dk Samia Mkurugenzi Wizara Ya Biashara Na Maendeleo Ya Viwanda Soud Saidi Amesema Wamekuwa Na Utaratibu Mzuri Wa Kununua Karafuu Kwa Kuhakikisha Wananunua Karafuu Zenye Kukidhi Viwango Vya Ubora
Jengo Hilo La Uwekezaji La ZSTC Lenye Ghorofa Tatu Linajumuisha Ghala, Milango Ya Biashara , Huduma Za Kibenki Na Limegharimu Shilingi Milioni 7.9 Za Kitanzania .