Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Abdallah amewataka Mawakili wapya kutekeleza kazi zao kwa kufuata sheria na taaluma.
Akizungumza katika Ukumbi wa Mahakama Kuu Tunguu wakati wa kuwaapisha Mawakili Wapya kumi na sita ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya Wiki ya Sheria Zanzibar. Amesema maadili ya kazi zao ni kusimamia haki na wajibu ili kutetea haki za Wananchi na kuisaidia Mahakama kutenda haki kwa Wananchi.
Amesema Mahakama imekuwa na Kamati ya Maadili na nidhamu ili kutekeleza kazi zake ipasavyo.
Mawakili wapya waliopatiwa vyeti katika hafla hiyo wameahidi kuendelea kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.
stories
standard