Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora Mhe Haroun Ali Sleman amesema matumizi ya Teknolojia katika utowaji wa huduma za Msaada wa Kisheria kutarahisisha upatikanaji wa haki kwa Jamii kwa wakati.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya Tano ya Wiki ya Msaada wa kisheria huko Mazizini Mhe Haroun amesema kwa Mwaka 2024 maadhimisho hayo yameratibiwa na Idara ya katiba na msaada wa Kisheria kwa kushirikiana na Shirika la Legal Serives Facility pamoja na Shirika la maendeleleo la umoja wa Kimataifa undp.
Amesema maadhimisho hayo yamekuja na kaulimbiu yenye kuhamasisha matumizi ya Teknolojia kwa lengo la kutoa huduma bora za Msaada wa Kisheria kwa Jamii kutokana na mabadiliko ya Teknologia yaliopo sasa.
Amefahamisha kuwa Wiki ya Msaada wa Kisheria itajumuisha shughuli mbali mbali ikiwemo Kampeni kwa Vyombo vya Habari, Kongamano la Vyuo Vikuu kuhusu masuala ya msaada wa kisheria, utowaji wa huduma za Msaada wa Kisheria ambapo kilele chake ni Tarehe 28 Mwezi huu katika Ukumbi wa Shekh Idrisa Abdul Wakili na Mgeni Rasmu anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi.