MAKONDA AWATAKA MAAFISA ARDHI KUBADILIKA

Makonda ziarani Tanga

  Mkaazi wa kijiji cha Mandera Kata ya Segera Wilayani Handeni Ndg. Mustafa Senkondo amejikuta akiangua kilio mbele ya katibu wa halmashauri kuu ya CCM taifa ,itikadi ,uenezi na mafunzo Paul Makonda , akiomba wapatiwe mashamba kwani wananchi wa eneo hilo hawana maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo.

   Akizungumza katika muendelezo wa ziara yake Mkoani Tanga akiwa kata ya Segera Mwananchi huyo amesema kuwa wananchi wa kijiji cha Jitengeni hawana eneo la kilimo na waliomba kupatiwa ekari 1000 kwenye  shamba la mkonge ila tangu 2007 mpaka sasa hakuna majibu .

  Awali kabla ya kuanza kusikiliza kero hizo za migogoro ya ardhi Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM taifa , itikadi , uenezi na mafunzo Paul Makonda aliwataka maofisi Ardhi kubadilika na kumrudia Mungu kwani , malalamiko ya migogogro ya ardhi yamekuwa ni mengi .

  Akijibu kuhusu mgogoro huo mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando, amesema kuwa suala hilo lipo ngazi ya wizara  kwa sababu eneo ambalo wanaomba wananchi hao mmiliki anamiliki kihalali na ana hati ya umiliki na watashughulikia changamoto hizo.

   Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM taifa , itikadi , uenezi na mafunzo Paul Makonda amekamilisjha ziara yake ya siku mbili Mkoani Tanga na anaelekea mkoani Kilimanjaro.

 

 

 

 

 

 

standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.