MABADILIKO YA SHERIA KUIMARISHA UTENDAJI

BARAZA LA WAWAKILISHI

Kamati ya kusimamia Ofisi za VIongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi imeshauri Serikali kuendelea kufanya tafiti kwa sheria mbali mbali ambazo zitatoa miongozo kwa Taasisi za umma ikiwa ni pamoja na kuimarisha suala la utowaji wa huduma

Akiwasilisha maoni ya Kamati hiyo kuhusiana na Mswada wa Sheria mbali mbali na kuweka masharti bora ndani yake Makamo mwenyekiti wa kamati hiyo Mh Maryam Thani juma amesema hatua hiyo itasaidia kukuza utendaji na utowaji huduma za uhakika

Wajumbe wa baraza la Wawakilishi wamesema marekebisho ya Mswada huo ni sehemu ya kuimarisha utowaji huduma bora kwa taasisi za umma na Binafsi.

Akitoa ufafanuzi wa hoja za Wajumbe hao Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk Mwinyi Talib Haji amewatoa hofu Wajumbe kuhusiana na suala la kuunganisha baadhi ya Taasisi zinazotekeleza majukumu yanayofanana kuwa walifanya utafiti wa kina na kugundua kuwa ufanisi utakaopatikana

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.