Habari

HALI YA VIFO VYA MAMA NA MTOTO IMEKUWA TATIZO NCHINI.

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Hassan Khamis Hafidha amesema hali ya Vifo vya Mama na Watoto imekuwa tatizo  Nchini kutokana na ukosefu wa Damu kwa Mama Mjamzito wakati wa kujifungua na kutohudhuria Kilini kwa wakati.

Akizungumza katika Mkutano maalum wa kutathimini Vifo vya Mama Wajawazito kati ya Wizara na Watendaji mbali mbali wa ndani na Nje ya Nchi Naibu Hafidhi amewataka kina Mama hao kutumia Lishe  bora ili kuwa na kiwango sahihi cha Damu ambacho kitaweza kumsaidia wakati wa kujiifungua.

WATENDAJI WA MAHKAMA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO.

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Shaaban amewataka Watendaji wa Mahkama kufanya kazi kwa ushirikiano ili kudoa migogoro baina yao na Wananchi.

Ameyasema hayo katika ziara ya kila Mwaka ya kuzitembelea Mahkama Jaji Khamis  amesema ni vyema kuwa na ushirikiano bora ili kuondokana na vitendo vya rushwa ambavyo vitaleta ufanisi katika kazi.

WAJASIRIAMALI KUREJESHA MIKOPO KWA WAKATI

Wizara ya uchumi wa Buluu na Uvuvi imehimizwa kuwasimamia Wananchi katika kurejesha Mikopo ya boti za Uvuvi inayotolewa kwa vikundi mbali mbali vya Wajasiriamali kwa lengo la kuwainua Kiuchumi ili iweze kuwanufaisha na wengine.

Wajumbe wa kamati ya Utalii Biashara na Kilimo   chini ya Mwenyekiti wake Mhe Mtumwa Peya Yussuf wametoa Rai hiyo wakati wakipokea Taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Wizara hiyo katika Kikao kilichowakutanisha Watendaji wa Wizara pamoja na Watendaji wa Benki ya CRDB.

WANACCM WAMETAKIWA KUKILINDA CHAMA

Chama Cha Mapinduzi CCM kimesema hakitasusia maridhiano na Vyama vya Upinzani Nchini kwenye jambo lolote la kujenga na lenye Maslahi kwa Taifa na Wananchi wake.

Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Katibu  Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Dkt.Emmanuel Nchimbi wakati akizungumza na Wanachama alipowasili kwa mara ya kwanza Makao Makuu Dodoma Tangu kuteuliwa.

Aidha Dkt.Nchimbi,amewataka wana CCM kuendelea kukilinda Chama na mshikamano uliopo kwa sasa.

DKT. SAMIA KUTARAJIWA KUFANYA ZIARA NCHINI INDONESIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya Kitaifa Nchini Indonesia kwa lengo la kukuza na kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia na kuimarisha uhusiano wa Kiuchumi kati ya Nchi hizo mbili kupitia Sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Nishati, Madini, Elimu, Uchumi wa Buluu na ulinzi.

JUMUIYA YA MUZDALIFA IMESHAURI TAASISI ZA KIJAMII KUSHIRIKIANA

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Muzdalifa Farouk Hamad amesema ameshauri Taasisi za Kijamii kushirikiana na kuwa na malengo ya pamoja katika kuifikia Jamii.

Akikabidhi Msaada wa vitu mbambi mbali kwa Masheha na Yatima katibu Farouk amesema malengo ya pamoja yataisaidia Serikali katika kukuza ustawi wa Jamii

Amesema hayo wakati akikabidhi Msaada huo  na kuipongeza Serikali kwa kuendelea kuwapunguzia ushuru katika mambo yanayohusu Jamii.

MAKONDA AWATAKA MAAFISA ARDHI KUBADILIKA

  Mkaazi wa kijiji cha Mandera Kata ya Segera Wilayani Handeni Ndg. Mustafa Senkondo amejikuta akiangua kilio mbele ya katibu wa halmashauri kuu ya CCM taifa ,itikadi ,uenezi na mafunzo Paul Makonda , akiomba wapatiwe mashamba kwani wananchi wa eneo hilo hawana maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo.

   Akizungumza katika muendelezo wa ziara yake Mkoani Tanga akiwa kata ya Segera Mwananchi huyo amesema kuwa wananchi wa kijiji cha Jitengeni hawana eneo la kilimo na waliomba kupatiwa ekari 1000 kwenye  shamba la mkonge ila tangu 2007 mpaka sasa hakuna majibu .

WANANCHI HANDENI WALIA NA TANESCO

    Wananchi Wilayani Handeni Mkoani Tanga wamelalamika kukosa huduma ya umeme wa uhakika kwa kukatika mara kwa mara, huku wakiliomba shirirka la umeme Tanzania (TANESCO) kutoa taarifa kwa uwepo wa tatizo hilo .

   Wakizungumza kwenye kikao maalum kilichoitishwa na uongozi wa kata ya Chanika Wilayani hapa , Wananchi hao wamesema kuwa imefika hatua hata vifaa vyao vya ndani vinaungua kutokana na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara.

VIONGOZI WA CCM WAMETAKIWA KUACHA KUHUJUMIANA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, amewataka Viongozi wa Chama hasa wa  Matawi kuwashawishi Vijana kujiunga na CCM  ili kiweze kupata Wanachama wengi na kukiwezesha kushinda katika uchaguzi wa Mwaka 2025.

MFUKO WA MAAFA KUWEZESHWA ILI KUKABILIANA NA MAAFA YANAPOTOKEA.

Kamati ya kudumu ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi imeishauri ofisi za Makamu wa pili ya Rais kupitia Kamisheni ya kukabiliana na Maafa kuaandaa utaratibu wa kuupatia fedha Mfuko wa kukabiliana na Maafa ili yanapotokea maafa Serikali iwe na uwezo wa kuwasaidia Wananchi wake kupitia Mfuko huo.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.