Habari

SMT NA CUBA ZIMESAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamuhuri ya Cuba zimesaini makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya Kilimo, Afya, na Elimu ili kuongeza tija ikiwemo kukiongezea nguvu Kiwanda cha kuzalisha Dawa za kuulia Wadudu kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani.

Makubaliano hayo yamesainiwa Jijini Dar Es Salaam na wawakilishi wa Tanzania na Cuba na kushuhudiwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt Philip Mpango na Makamo wa Rais wa Cuba Salvador Veldes ikiwa ni sehemu ya ziara ya Kiongozi huo Nchini.

JAMII KUPIGA VITA SUALA LA UDHALILISHAJI KWA WANAWAKE NA WATOTO.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala bora Omar Haji Gora ameitaka Jamii kuhakikisha wanapiga vita suala la udhalilishaji  kwa Wanawake na Watoto ambalo  linaleta athari katika Jamii .

Akifungua mafunzo ya ushauri nasaha kwa wahusika wa masuala ya udhalilishaji Gora amesema endapo juhudi  zitachukuliwa  tatizo hilo linaweza kuondoka na  kupatiwa ufumbuzi katika Jamii.

SMZ IMEOMBWA KUWEKA KODI RAFIKI KWA WAJASIRIAMALI LIMBANI.

Wafanyabiashara katika Soko la Wajasiriamali Limbani Wete, wameiomba Serikali kuweka Kodi rafiki pamoja na kusimamia mnada wa Bidhaa Sokoni hapo ili kuwaondoshea usumbufu wanaoupata Wanunuzi.

Wametoa ushauri huo wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Wete Dkt Hamad Omar Bakar ya kuangalia mwenendo wa Biashara katika Soko hilo.

Wamesema maendeleo ya Biashara zao zinakwamisha kutokana na kodi na kushindwa harakati zao za kujiongezea kipato.

UJENZI WA BANDARI JUMUISHI YA MANGAPWANI UTAHUSISHA BANDARI ZA KISASA

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi imesema Ujenzi wa Bandari Jumuishi ya Mangapwani utahusisha Bandari za kisasa, Miundombinu na maeneo ya uwekezaji.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi huo mbele ya kamati ya Bajeti Waziri wa ujenzi, mawasiliano na uchukuzi Dkt. Khalid Salim Mohamed amesema ujenzi huo utajumuisha Bandari ya mizigo mchanganyiko, Bandari ya Mafuta na Gesi, eneo la kuwekea Makontena, kuhifadhia Mizigo, Barabara, Viwanda, Makaazi, Elimu, michezo na maeneo mengine.

KAMISHENI YA WAKFU ZANZIBAR YATOA SADAKA YA NYAMA KUTOKA SAUDI ARABIA

   Kamisheni ya wakfu na mali ya amana Zanzibar imetoa sadaka ya nyama iliyotoka Saudi Arabia kwa wakuu wa wilaya wa Unguja na Pemba ili kuwapatia wananchi wasiojiweza .

   Akikabidhi sadaka hiyo kaimu mkuu wa Divisheni ya zaka na misaada kamisheni ya wakfu na mali ya amana Zanzibar Ndg. Hassan Ali Kombo kwa niaba ya katibu mtendaji amesema watahakikisha sadaka hiyo inawafikia waliokusudiwa ikiwemo watu wenyemahitaji maalum , na taasisi za kulelea watoto yatima .

WANAWAKE ZANZIBAR WATAKIWA KUTUMIA FURSA MBALI MBALI KUJIKWAMUA NA UMASIKINI

   Waziri wa Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amewataka wanwake kuzitumia fursa mbali mbali zinazowafikia kujiinua kiuchumi na kuweza kujikomboa na umasikini . 

    Wito huo ameutoa katika uzinduzi wa mradi wa kuwawezesha wanawake kiuongozi katika mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika huko katika Shehia ya Kambini chokochwe Wilaya ya Wete Pemba na kuhudhuriwa na Balozi wa Canada nchini Tanzania Ndg. Kyle Nunas.

 Amesema wanawake ni chachu ya maendeleo katika jamii hivyo fursa zinazpotokea ziwaongezee weledi .

BODI YA VILEO YATKIWA KUONDOSHA KASORO ZA UTOAJI WA HUDUMA KWA WAGENI

   Wizara ya Utalii na mambo ya kale Zanzibar imeitaka bodi ya vileo kuondosha kasoro zilizopo katika utoaji wa huduma kwa wageni ili kulinda biashara ya utalii.

   Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Simai Mohamed Said ameyaeleza hayo alipokuwa akizungumza na wadau wa sekta ya utalii huko Kikwajuni Mjini Zanzibar ambapo amesema uwepo wa kasoro katika sekta hiyo unaweza kuathiri harakati za uchumi ambao kwa kiasi kikubwa unategemea sekta ya utalii.

WAJASIRIAMALI JIMBO LA UZINI WAOMBA KUPATIWA MITAJI

   Zaidi ya vikundi 13  vya wajasiriamali wanawake katika Jimbo la Uzini wamewaomba viongozi wao kuweza kuwasaidia mitaji ya kuviendeleza vikundi vyao ili viwaletee tija na kujikwamua na maisha .

    Wakitoa maombi yao kwa Viongozi wa Jimbo hilo huko Mitakawani , wamesema vikundi vingi vinashindwa kupiga hatua kutokana na kukosa mitaji ya kutosha , hivyo wamewaomba kuwaunga mkono ili waweza kufanya shughuli zao kwa ufanisi .

ZBS WATAKIWA KUENDELEA KUZINGATIA VIWANGO VYA BIDHAA NCHINI

  Kamati ya Utalii Biashara na kilimo ya baraza la wawakilishi imeitaka Taasisi ya viwango Zanzibar ZBS kuendelea kuzingatia viwanzgo vya bidhaa nchini ili kusaidia Serikali kudhibiti bidhaa zilizokwisha wa muda wa matumizi kuingizwa nchini .

    Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kamati ya utalii , biashara na kilimo ya Baraza la wawakilishi makamo mweyeketi wa kamati hiyo Mh. Hussein Ibrahim Makungu , amaesma taasisi hiyo ina umuhimu kwa serikali na kubaini matatizo na kutafutia ufumbuzi ili kuwafanya wannchi kubaki salama.

WAMILIKI NA WALIMU SHULE BINAFSI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA

   Waziri wa elimu na mafunzo ya amali Zaznzibar Mh. Leila Mohamed Mussa amewataka wamiliki na walimu wakuu wa shule binafsi kisiwani Pemba kuhakikisha wanashirikiana na Wizara katika kupanga mipango yao ya kitaaluma.

   Waziri Leila ametoa wito huo huko katika ukumbi wa Chuo cha mafunzo ya amali Vitongoji Chakechake Pemba alipokutana na wamiliki  hao pamoja na walimu wa shule hizo kwa lengo la kujadiliana juu ya msauala mbalimbali ya maendeleo ya elimu katika sekta binafsi.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.