Habari

CHINA NA ZANZIBAR KUONGEZA WIGO KATIKA FANI ZA BAHARI

       Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar na Wizara ya Maliasili ya Jamuhuri ya Watu wa China zimetilian saini hati ya mashirikiano na bahari ya Jamuhuri ya Watu wa China ili kuendeleza vyema sera ya Uchumi wa Buluu.

       Waziri wa fedha na mipango Zanzibar Dkt. Saada Mkuya Salum amesema hayo kwa niaba ya Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe .Shaabani Ali Othman huko Maisara amesema Zanzibar ina fursa nyingi za kutekeleza ajenda ya uchumi wa buluu hivyo amewataka Wananchi kutumia fursa hiyo

BENBELA KUADHIMISHA MIAKA MIA TOKEA KUASISIWA KWAKE

      Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Bembela Ndg.Ramla Moh'd Ramadhan amesema kuwa Skuli ya Benbela imefanya vyema tokea kuanzishwa kwake Miaka mia na haijawahi kutetereka.

      Akizungumzia tamasha la kuadhimisha Miaka mia moja ya mafanikio tokea kuanzishwa kwa Skuli hiyo Ndg.Ramla amesema kuwa katika mikondo tofauti iliyopitia Skuli hiyo bado inaendeleza ubora wake kwa kutoa vipaji.

JAMII YATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI JUU YA UGONJWA WA MALARIA

      Mashehe na Maimam wamekumbushwa kutoa elimu kwa Waumini wao juu ya athari za ugonjwa wa Malaria ili jamii iweze kuchukuwa tahadhari.

     Akitoa Elimu kwa imam wa Mashehe wa Wilaya ya Mjini Afisa kitengo cha malaria Ndg.Mwinyi Khamis amesema kumekuwa na ongezeko la ugonjwa huo na tayari baadhi ya watu wamepoteza maisha.

     Ndg.Mwinyi amesema elimu hiyo ni muhimu kwa Viongozi hao wa Dini kutoa elimu kwa waumini wao ili kuwa na njia za kujikinga,

CHINA KUTOA UFADHILI WA FANI YA VIUMBE WA BAHARINI KWA WAZANZIBARI

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Maliasili wa China Mhe. Sun Shuxian na ujumbe wake.

   Dkt Mwinyi amefanya mazungumzo hayo Ikulu Mjini Zanzibar na kuishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa kuendelea kuisadia Zanzibar katika Sekta mbali mbali ambayo imeifanya kuwa na maendeleo.

DKT HUSSEIN MWINYI AMERIDHIA KUJIUZULIU WAZIRI SIMAI

Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk Hussein Ali Mwinyi ameridhia ombi la kujiuzulu kwa Waziri wa Utalii na mambo ya kale Mhe Simai Mohammed Saidi kuanzia leo.

Akithibitisha kauli ya aliyekuwa Waziri wa utalii na mambo ya kale Msemaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Cherlse Hilari.

WAANDISHI WA HABARI KUVITANGAZA VIVUTIO VYA UTALII PEMBA.

Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba wametakiwa kutumia nafasi yao katika kuvitangaza vivutio vya utalii Kisiwani humo ikiwa na lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali kukifunguwa  Kisiwa hicho Kitalii na kuimarisha uchumi wa Nchi.

TUZO ZA WAFANYAKAZI BORA ZBC ZATOLEWA

     Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC Ndg.  Ramadhan Bukini amewahimiza Watendaji wa Shirika hilo kuongeza juhudi na ufanisi katika kazi ili kuyalinda mafanikio yaliyopatikana.

     Akizungumza katika hafla ya kugawa tuzo kwa vipindi na Watangazaji bora pamoja na kuwapongeza Wafanyakazi bora wa Shirika la Utangazaji kwa Mwaka 2023/2024 amesema mafanikio yaliyopatikana yanatokana na ushirikiano wa pamoja wa Idara zote za ZBC na kwamba kuna haja ya kuyaendeleza ili kulinda mafanikio hayo.

TANZANIA NA INDONESIA KUKUZA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA NA UCHUMI

    Tanzania na Indonesia zimekubaliana kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Nchi hizo kwa kukuza ushirikiano katika Sekta za Uchumi wa Bbuluu, Kilimo, Madini, Afya Diplomasia Biashara na uwekezaji.

    Katika ziara ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Ttanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Nchini Indonesia ambapo Viongozi hao wanashuhudia mabadilishano ya hati 4 za makabaliano na barua moja ya kusudio kati ya Nchi hizo.

SUALA LA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI LINAHITAJI MUDA

  Mamlaka ya utafutaji na uchimabaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar imesema suala la utafutaji wa rasilima hizo unahitaji utafiti wa kina ili kukamilika kwake na kupata matokeo sahihi kwa zoezi hilo.

      Wakitoa uwelewa kwa Watendaji wa Shirika la Mawasiliano Zanzibar kuhusu hatua iliyofikia Mkurugenzi idara ya data Ndg.Mohamed Salum na Meneja wa mamlaka hiyo Ndg. Khamis Juma wamesema hadi sasa kumetangazwa uwepo wa vitalu na maandalizi yake ni kuvitangaza kwa ajili ya wawekezaji kuekeza.

ZECO YAJIPANGA KUONDOA KERO YA UMEME

    Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) linajenga laini mpya kutoka Mtoni kwenda vituo vyengine ili kuondokana na  tatizo la kukatika ovyo kwa umeme kwa baadhi ya maeneo.

      Akizungumza wakati mafundi wa ZECO wakiendelea na matengenezo kwa laini ya Dole na Maruhubi, Mhandisi ugavi wa Shirika Ndg. Ali  Kassim Fumu, amesema kumekuwa na jitihada ya kulipatia ufumbuzi tatizo hilo kwa kipindi kifupi kijacho.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.