Habari

ZAWA YAENDELEA NA JITIHADA ZA KUREJESHA HUDUMA ZA MAJI MJINI

      Malaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) imesema inaendeelea na jitihada za kurudisha huduma ya Maji iliokosekana takriban wiki mbili ndani ya eneo la Mkoa wa Mjini.

WAHASIBU WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI ZAO

     Watendaji wa Taasisi ya Wahasibu Wakaguzi na Washauri elekezi wa kodi Zanzibar ( ZIAAT ) wamesisitizwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi zao ili kuepuka malalamiko yanayoweza kuathiri utendaji wao wa kazi.

KAMATI YA SIASA YA JIMBO LA MICHEWENI LIMEFANYA ZIARA KATIKA MIRADI YA KIMKAKATI KATIKA JIMBO HILO

        Kamati ya Siasa ya Jimbo la Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, imefanya Ziara katika miradi  ya kimkakati  katika  Jimbo hilo ili kuuangalia maendeleo na matatizo yanayojitokeza katika  miradi hiyo.

      Kamati hiyo ikiongozwa na Mbunge  wa Jimbo la Micheweni  Mh.Abdi Hijja Mkasha pamoja na mwakilishi  wa jimbo hilo Mh. Shamata Shaame Khamis  

DKT.SAMIA AZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI WA BOTI NA VIZIMBA KANDA YA ZIWA

       Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa kuhakikisha wanawasimamia vyema Wavuvi waliopewa boti na vizimba ili kuhakikisha wanatumia zana hizo kwa matumizi sahihi ili kusaidia ukuaji wa sekta ya uvuvi na kupunguza uvuvi haramu.

       Rais Samia amesema hayo Jijini Mwanza katika  uzinduzi wa ugawaji wa vizimba 222 vya kufugia Samaki na boti za kisasa 55 kwa Wavuvi kanda ya Ziwa  wenye kauli mbiu  uchumi wa buluu ni fursa muhimu kwa Wananchi.

ZANZIBAR YAPONGEZWA KWA KUIMARISHA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi mdogo wa China Mhe. Zhang Zhisheng anayefanyia kazi zake Zanzibar, kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa utumishi Nchini.

Rais Dk Mwinyi amemshukuru Balozi Zhang kwa kudumisha na kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Zanzibar na China katika miaka mitatu ya utumishi wake Nchini.

SERIKALI IMESEMA HAITOMVUMILIA MTU YEYOTE ANAEASHIRIA KUFANYA VITENDO VYA UHALIFU.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema haitomvumilia  mtu yoyote anaeashiria kufanya vitendo vya uhalifu vitakavyoharibu Amani iliopo Zanzibar.

‘’ikumbukwe kuwa  Mapema Tarehe 27  huko Darajani Mitandao mbalimbali ya Kijamii  ilionyesha Mtu mmoja anaefahamika kwa Jina Yussuf Faki  Seif ambae pia ni Mkuu wa Oparesheni Mji Mkongwe akishambuliwa na virungu na Jamii ya Watu waliovaa Nguo za Kimasai ‘’

KAMPUNI YA SUMSANG KUVUTIWA NA UWEKEZAJI ZANZIBAR

Wawekezaji wa Kampuni ya Sumsang inayoshughulikia Ujenzi na Viwanda kutoka Jamhuri ya Watu wa Korea wameelezea kuvutiwa na fursa za uwekezaji zinazopatikana Zanzibar.

Kiongozi wa ujumbe huo wa Wawekezaji, Yonyi Yi, katika mazungumzo na Watendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar ZIPA huko Maruhubi na Wadau wa Uwekezaji, amesema wamejionea maeneo ambayo ni Kivutio kwa  kuanzisha Miradi mbali mbali ya Kiuchumi.

MAKONDA AZUIA UNUNUZI WA MAZAO KWA NJIA YA STAKABADHI

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda, ameagiza ununuzi wa Mazao ufanyike kwa Soko huria, na siyo stakabadhi Ghalani.

Ametoa agizo hilo katika Mkutano wa hadhara Mjini Bariadi, baada ya kupokea ombi la Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi kundo Andrea Mathew, aliyeomba ununuzi wa mazao yakiwemo choroko, Mbaazi na mengineyo yafanyike katika Soko huria ili kumnufaisha Mkulima.

WAMILIKI WA SHULE BINAFSI WATAKIWA KUACHA KUCHUJA WANAFUNZI KULINGANA NA UFAULU

     Afisa Elimu Mkoa wa Geita Ndg.Antony Mtweve amezitaka Shule za Serikali na Binafsi kuacha kuchuja Wanafunzi kulingana na ufaulu katikati ya mzunguko wa masomo kwani ni kinyume cha utaratibu wa Serikali na Sera ya Elimu.

     Amezungumza hayo wakati akitaja matokeo ya kidato cha nne kwa shule za Serikali na Binafsi Mkoani Geita, huku akisema ufaulu umepanda tofauti na Mwaka jana.

MADEREVA WAMETAKIWA KUFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

     Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiya ya Madereva Mkoa wa Kusini Pemba Mwalimu Ali Mohamed Shela, amewashauri Madereva wa Gari za Abiria Nchini kufuata sharia za usalama Barabarani na sio kuwaona Askari wakorofi wanaposimamia sharia hizo.

    Ushauri huo ameutoa wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa PESTA, huko katika Ukumbi wa Skuli ya Madungu Maandalizi  Chake Chake.

   Amesema zipo sharia mbali mbali iwapo zikifuatwa ipasavyo basi Madereva hawana cha kupeleka kwa Tajiri, kutokana na uzidishaji wa Abiria wanaoufanya.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.