Habari

SMZ NA SMT ZAENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WAPIGANAJI NCHINI

     Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimesema zinaendelea kuunga mkono juhudi za Wapiganaji kwa kuwajengea uwezo ili kufikia malengo ya Serikali.

     SMZ na SMT  akifunga Mafunzo ya Wanafunzi wa Uhamiaji wa kozi ya uendeshaji vyombo vidogo vidogo na uzamiaji, Naibu Meya wa Magharibi b,Ndg Khadija Omar Ngarama, amesema hatua hiyo itasaidia Wapiganaji kufanya kazi zao kwa urahisi.

WATENDAJI WATAKIWA KUZIFANYIA KAZI SHERIA MPYA ZILIZOTIWA SAINI KWA KWA MASLAHI YA WANANCHI

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka Watendaji kuzifanyia kazi sheria mpya zilizotiwa saini kwa kwa maslahi ya Wananchi.

RAIS SAMIA AWATAKA MAHAKIMU NA MAJAJI KUTENDA HAKI

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan,amesema Serikali itaendelea kuchukua  hatua za kuimarisha utendaji kazi wa Mahakama ikiwemo  matumizi  ya Tehama na pia amewataka Majaji na Mahakimu kuishi katika misingi ya Viapo vyao kwa  kutenda haki.

   Rais Samia ameyasema hayo Jijini Dodoma  wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya sheria Nchini inayobebwa na kaulimbiu isemayo Umuhimu wa Dhana ya Haki Kwa Ustawi  wa Taifa na nafasi ya Mahakama na Wadau Katika Kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki.

DKT.WMINYI AWATAKA VIONGOZI KUFANYA KAZI KWA BIDII

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Viongozi kufanya kazi ya kuwatumikia Wananchi kwa mujibu wa sheria.

     Akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi aliowateuwa hivi karibuni huko katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar Dkt Mwinyi amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza fursa hasa katika sekta muhimu kwa uchumi ikiwemo sekta ya utalii.

SERIKALI KUHAKIKISHA HUDUMA ZA BIMA ZINAPATIKANA HADI VIJIJINI

Serikali imesema itaendelea kuhakikisha Bidhaa na huduma za Bima mbalimbali zinapatikana Nchini hususani katika maeneo ya Vijijini lengo likiwa ni kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na huduma ya Bima Nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Saada Mkuya wakati wa Uziniduzi wa Kampuni ya Bima ya First United Takaful.

Amesema Serikali zote mbili zinaendelea kuweka Mazingira wezeshi kwa Taasisi au Mtu anayetaka kufanya uwekezaji katika sekta ya Bima Nchini

SIKU YA SHERIA LENGO NI WANANCHI KUWA KARIBU NA MAHAKAMA

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Khamis Ramadhan amesema Siku ya sheria inalengo la kuwaelimisha Wananchi kuhusu Mahkama pamoja na kuwaweka karibu na katika utoaji wa huduma bora na upatikanaji wa haki kwa wakati.

Akizungumza na Waandishi wa Habari huko Tunguu amewataka Wananchi na Wadau wa Mahkama kujitokeza katika maadhimisho ya siku ya sheria ambayo itafanyika mwanzoni mwa Mwezi wa Pili Mkoa wa Kusini Unguja

Ameeeleza kuwa siku ya Sheria itajumuisha mambo mbali mbali ikiwemo utoaji wa Elimu, Matembezi na uchangiaji Damu kwa hiari.

ZSSF KUSIMAMIA MIRADI KUWA CHACHU YA UKUAJI WA UCHUMI

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF umehimizwa kuendelea kusimamia kwa karibu Miradi mbali mbali ya maendeleo wanayoitekeleza ili iweze kukamilika kwa wakati na kuwa chachu ya ukuaji wa Uchumi. 

Wajumbe wa kamati ya Bajeti ya Baraza la wawakilishi chini ya Mwenyekiti wake Mhe Mwanaasha Khamis Juma wametoa maelekezo hayo katika ziara ya kukagua na kupokea Taaarifa ya utekelezaji wa Miradi mbali mbali ikiwemo Kituo cha Mabasi Kijangwani, eneo la maegesho ya Magari Darajani na eneo la Biashara Mbweni ambayo inatekelezwa na Mfuko huo.

SMT KUFANYA TATHIMI YA MAENEO KUKABILIANA NA ATHARI ZA KIMAZINGIRA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta imeanza kufanya tathmini Nchi nzima kubainisha maeneo yanayohitaji kufanyiwa maboresho kukabiliana na athari za Kimazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtambwe Mhe. Khalifa Mohammed Issa aliyetaka kujua lini Serikali itafanya utafiti kuyabaini maeneo yaliyoathiriwa na mabadiliko ya Tabianchi.

SMZ KUWAFUNGIA MADUKA WANAOUZA SUKARI KINYUME NA BEI ELEKEZI

Wafanya Biashara wa Bidhaa za Vyakula wametakiwa kufata maelekezo ya Serikali katika kuendesha Biashara zao.                        

Akizungumza na Wafanya Biashara hao katika ukaguzi wa Bei za Vyakula  Mkurugenzi wa kumlinda Mtumiaji na udhibiti wa  Bidhaa Bandia kutoka tume ya ushindani halali wa biashara Eliar Emmanual Juma 

WAANDISHI WA HABARI WAMETAKIWA KUTUMIA VIZURI TAALUMA ZAO

     Waandishi wa Habari wametakiwa kutumia vizuri Teknolojia ya Habari ili kuihabarisha Jamii kuhusu takwimu za Sensa ya Watu na makaazi ya Mwaka 2022 na kuwepo matumizi sahihi ya Takwimu hizo.

     Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Ndg. Beno Malisa, wakati akifungua Semina kwa Waandishi wa Habari wa Mikoa ya Mbeya, Iringa na Songwe kuhusu usambazaji na uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.