Habari

SERIKALI YAJIPANGA KUPAMBANA NA SARATANI

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi,amesema Serikali inadhamiria kuongeza mikakati ya kulinda mazingira ili kukabiliana na ongezeko la Magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Saratani.

    Akizungumza katika Kikao cha uwekezaji  wa Sekta ya Afya kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Saratani Nchini huko katika Hoteli ya Hyatt Regency, Dar- es- salaam, amesema  Saratani ni Ugonjwa unaowaathiri Watu wengi Ulimwenguni.

WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUIBA MAFUTA MWANGAPWANI

Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja inawashikilia Watu Wawili kwa tuhuma za kutaka kuiba Mafuta kwenye Gari ya Miradi ya Ujenzi wa Barabara katika Bandari ya Mwangapwani.

Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo huko Mahonda Kamanda wa Polisi Mkoa huo Kamishna Msaidizi wa Polisi Daniel Shila amesema Jeshi hilo lkiwa katika Doria zake huko eneo la Kitope kwenye Maegesho ya Gari ya Kampuni ya Orkun, limewakamata Watu hao wakiwa na Madumu na Mipira ya kunyonyea Mafuta kwa nia ya kutaka kuiba Mafuta.

SERIKALI KUFANYA MAREKEBISHO SERA YA MAMBO YA NJE YA MWAKA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe. Ali Suleiman Ameir na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Yusuf Makamba wamesema kwa misingi ya Utawala bora Serikali inapotaka kutunga Sera lazima ipate maoni ili Sera inayotungwa iwe bora na izingatie maoni ya Wananchi na Wadau.

SERIKALI KUWAFUTIA LESENI WATAKAOKIUKA BEI ELEKEZI YA SUKARI

Bodi ya Sukari Nchini imesema itachukua hatua kali ikiwemo kufuta Leseni kwa Mawakala na Wafanyabiashara watakaoshindwa kuzingatia Bei elekezi iliyotolewa na Serikali kwa Bidhaa hiyo.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar Es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari, Profesa Kenneth Bengesi wakati wa zoezi la kupakia Sukari kwenye Bandari kavu ambayo inapelekwa Mikoani ili kukabiliana na uhaba wa Bidhaa hiyo.

ZAECA KUFANYA UCHUNGUZI DHIDI YA WAFANYAKAZI WA MKATABA

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Shaabani Ali Othmani ameitaka Mamlaka ya kuzuia na kupambana na Rushwa kufanya uchunguzi dhidi ya Wafanyakazi wa Mkataba ambao walikuwa wanaohusika na ukusanyaji wa Mapato katika hifadhi za Chabamca  kutokana na kupoteza kwa mapato katika maeneo hayo.

SMT KUPATA ZAIDI YA SHILINGI TRILIONI 2 KWA BIASHARA YA KABONI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali inatarajia kupata wastani wa Shilingi Trilioni 2 nukta 4 kutokana na Biashara ya Kaboni ambazo zitachangia kuimarisha pato la Taifa.

Dkt. Jafo ameliarifu Bunge wakati akijibu swali la Mbunge wa Buhigwe Mhe. Kavejuru Felix aliyetaka kujua biashara ya Kaboni katika misitu ya asili na ya kupanda imechangia kiasi gani kwenye pato la Taifa tangu iingie Nchini.

SMT KUJENGA UKUTA ENEO LA NUNGWI

    Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza kujenga ukuta katika eneo la Nungwi Zanzibar kwa ajili ya kuzuia maji ya Bahari kuingia kwenye makazi ya Wananchi kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

    Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ameyasema hayo  wakati akijibu maswali Bungeni Jijini Dodoma.

   Katika hatua nyingine Mhe.Khamis ametoa  rai kwa Wananchi kuacha kufanya shughuli zinazoharibu mazingira ya Visiwa.

UJENZI WODI YA WAZAZI KATA YA MNALI MANISPAA YA LINDI KUANZA

    Wananchi wa Kata ya Mnali Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wameishukuru Serikali kwa kuanza Ujenzi wa Jengo la Wodi ya Wazazi katika Zahanati ya Kata hiyo.

    Hatua ya Serikali kujenga Wodi hiyo  imekuja baada ya kuwa na tatizo la ufinyu wa Chumba cha kujifungulia katika Zahanati hiyo  hali iliyowalazimu Wananchi kujitolea  kuanza kujenga Wodi ya Miti pembezoni mwa Zahanati hiyo  Mwaka 2022.

JAMII YATAKIWA KUENDELEA KUTUMIA MATOKEO YA UTAFITI

    Wananchi wamehimizwa kuthamini kazi zinazofanywa na watafiti zinalenga  kuendeleza utalii wa mazingira juwa endelevu ili zanzibar kuwa kivutio cha wageni na wakaazi wake. 

ZECO YAN'GARISHA KISIWA PANZA

    Zaidi ya Wananchi 103 wa Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani wameanza kutumia Umeme wa ZECO  baada ya Nyumba zao Shirika kukamilisha utaratibu.

    Akizungumza na ZBC, Afisa Mawasiliano na huduma kwa Wateja Shirika la Umeme Zanzibar Tawi la Pemba (ZECO), Ndg.Haji Khatib Haji amesema baada ya Wananchi kupatiwa Elimu na kushajiliwa tayari Wananchi 103 wameanza kunufaika na huduma hiyo.

   Amesema Wananchi wataweza kunufaika na Umeme kwa ajili ya kusomea muda wa ziada, kuhifadhi samaki wao ikizingatiwa

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.