Habari

MAFUNZO KWA VIJANA HUSAIDIA KUONGEZA KASI YA MAENDELEO NCHINI

   Vijana waliomaliza Mafunzo ya U/Riport wametakiwa kuwa Mabalozi kwa Vijana Wenzao katika kuwajengea uwezo  kupitia fursa wanazozipata kutoka Taasisi mbalimbali.

   Akizungumza katika Mkutano wa Kuwaaga Vijana Mabalozi wa Program hiyo katika Ukumbi wa Takwimu Mazizini Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana Shaib Ibrahim Wizara ya Habari imeamuwa kujenga Vituo Vinne vitakavyotowa Taaluma kupitia Vijana hao kwa lengo la kuwajenga Kitaaluma

VINAJA UVCCM WATAKIWA KUWA WAZALENDO

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa  NEC Leila Burhani Ngozi  amewataka  Wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu kuzidisha uzalendo katika Vyuo  ili kuwa  Waadilifu kwa Maendeleo ya Taifa,

    Akifunga Kongamano la Wasomi vyuo na Vyuo Vikuu Seneti Mkoa wa Magharib Tawi la Mwalimu Nyerere Bububu  amesema Kijana Mzalendo ni yule mwenye kujitolea kutetea maslahi ya Taifa kwa faida ya Kizazi cha sasa na Kijacho.

WANANCHI JAMII YA KIMASAI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA NGORONGORO WAFANYA TAMASHA LA KIMILA NA KIUTAMADUNI

     Wananchi wa jamii ya kimasai wanaoishi ndani ya hifadhi ya Ngorongoro wamefanya tamasha la kimila la kiutamaduni huku wakisema kwamba wataendelea kuhama kwa hiyari kuelekea katika Kijiji cha Msomera na maeneo mengine nchini Tanzania.

CCM INAJUKUMU LA KUTATUA MATATIZO MBALIMBALI YA WANANCHI

    Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Mohamed Dimwa  amewataka Wananchi  kuwasilisha matatizo yao wanayokumbana nayo wapokwenda katika Taasisi za Serikali kufuata huduma ili kuona yanapatiwa ufumbuzi.

WASIMAMIZI WA MIRADI YA SERIKALI WAHIMIZWA KUMALIZA MIRADI YAO KWA WAKATI

    Wahandisi na Wasimamizi wa Miradi ya Kimkakati ya Serikali wametakiwa kuzidisha umakini katika kusimamia Miradi hiyo ili kumalizika kwa Wakati na viwango bora.

BIDHAA ZILIZOSAFIRISHWA ZANZIBAR KWA MWEZI WA MEI 2024 ZAONGEZEKA

   Bidhaa zilizosafirishwa Zanzibar kwa Mwezi wa Mei 2024 zilikuwa na Thamani ya Shilingi Bilioni 5 Nukta 0 Thamani ambayo imeonekanwa kuongezeka.

   Akiwasilisha Takwimu za Biashara za Kimataifa kwa Mwezi huo Mtakwimu kutoka kitengo cha Takwimu za Biashara na Kodi Ndg.Asia Salum Rashid amesema Kundi la Vyakula na Wanyama hai linaongoza kwa Thamani yote ya usafirishaji wa Bidhaaa ambapo bidhaa zilizosafirishwa kwa Makundi maalumu ni Chakula  Wanyama na aina nyengine za  Bidhaa za Viwandani.

MADAKTARI WA UPASUAJI WATAKIWA KUJIUNGA NA CHAMA CHA MADAKTARI WA UPASUAJI NCHINI

   Kiongozi wa Timu ya 33 ya Madaktari kutoka China Dkt.Jiao Cheng amesema wataendelea kushirikiana na Madakatari wa Upasuaji Nchini Tanzania kwa kupeana taalamu kwa lengo la kutoa huduma ubora kwa Wananchi.

   Akizungumza katika Mkutano wa 29 wa Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania uliofanyika Mkoani Morogoro ambao umewashirikisha Madaktari mbali mbali wa Upasuaji Nchini, Dkt.Jiao amesema Mkutano huo unawezesha kupeana utaalamu zaidi katika huduma za Upasuaji.

AMANI NA TULIVU NI NGAO YA NCHI ZA AFRIKA NA DUNIANI KOTE

   Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson, amesema amani, tulivu na usalama ndio ngao ya Nchi za Afrika na Duniani kote.

    Akizungumza katika muendelezo ya Ziara yake na Wabunge wa Mabunge Duniani, amesema Nchi nyingi Barani Afrika zina Migogoro na vita vya Wenyewe kwa Wenyewe na kusababisha athari mbali mbali.

   Amesema Umoja huo unakusudia kujadili Maeneo yote yenye matatizo mbali mbali ikiwemo  vita na kuyatafutia ufumbuzi.

ZIC IKISHIRIKIANA NA MWANAMKE INITIATIVE FOUNDATION WAKABIDHI MSAADA WA VITABU KWA MKOA WA KUSINI UNGUJA

   Shirika la Bima Zanzibar ZIC likishirikina na Taasisi ya Mwanamke Initiatives Fondation wamekabidhi msaada wa Vitabu vya Mitaala kwa Skuli za Secondari ili kukuza kiwango cha ufaulu katika Skuli za Mkoa ya Kusini Unguja. 

WAZIRI MKUU AWATAKA WAKUU WA MIKOA NA WAKUU WA WILAYA KUANZISHA ULINZI KWA WATU WENYE UALBINO

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha kila Halmashauri inaanzisha msako maalum kwa Watu wenye Ualbino.

   Mhe.Kassim Majaliwa ametoa Wito huo Bungeni Jijini Dodoma wakati akitoa Taarifa kuhusu kupinga ukatili dhidi ya Watu wenye Ualbino wakati wa Kipindi cha Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

    Aidha Waziri Mkuu amewataka  Waganga wa Jadi Nchini kote  kushiriki kikamilifu katika Kampeni za kupinga Mauaji ya Watu wenye Ualbino

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.