Habari

SERIKALI ITAENDELEA KUTHAMINI MCHANGO WA WASANII WAKONGWE NCHINI

    Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Baraza la Sanaa Sensa, Filamu na Utamaduni Zanzibar imesema bado inathamini mchango mkubwa unaotolewa na Wasanii katika kuhakikisha Sanaa inaimarika Nchini.

   Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Idara ya Utamaduni Zanzibar Dkt.Omar Salum Muhammed baada ya Ziara yakuwatembelea baadhi ya Wasanii Wakongwe walioitumikia saana hapa Zanzibar , ambapo amesema niwajibu wao kama Idara kupitia Wizara kuandaa Ziara ya kuwatembelea Wasanii Wakongwe ili kujuwa afya zao pamoja kuthamini jitihada zao.

TAASISI YA BIG PHILANTHROPY YA UINGEREZA KUSHIRIKIANA NA SMZ MPANGO WA LISHE MASHULENI

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka Taasisi ya Big Philanthropy ya Uingereza kushirikiana na Serikali kwa mpango wa lishe Skuli katika kupunguza Utoro na kuongeza Ufaulu.

   Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Big Win Philanthropy, Dkt. Kesete Admasu na Ujumbe wake waliofika Ikulu Jijini Zanzibar.

WIZARA YA KAZI KWA KUSHIRIKIANA NA ILO WAANDAA MIFUMO WEZESHI YA AJIRA

   Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji imejipanga kuondosha tatizo la ukosefu wa Ajira Nchini kwa kuandaa Mifumo itakayoendana na matakwa ya Waajiriwa itakayowahamasisha kufanya kazi kwa Ufanisi.

    Huyo ni Mhe.Sharif Ali Sharif, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji, akifungua Warsha juu ya Uaandaaji wa Mifumo ya Soko la Ajira huko Golden Tulip Waziri huyo ameuhakikishia Umma kwamba Mifumo hiyo itakapokamilika itaondosha urasimu katika Soko la Ajira.

KUIMARIKA KWA BIASHARA KUTASAIDIA KUKUWA KWA UCHUMI WA AFRIKA

    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah amesema kuimarika kwa biashara katika eneo la Afrika kutasaidia kupatikana fursa zaidi na bara hilo kuweza kujitegemea kiuchumi.

     Akifungua mkutano wa 3 wa Mawaziri na mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri wa Eneo huru la Biashara Afrika (afcfta) huko katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip uwanja wa ndege Mkoa wa Mjini Magharibi, amesema hatua hiyo itakuza nguvu na dhamira ya viongozi na waasisi wa nchi zao katika kujenga nguvu ya pamoja na kukuza uchumi.

MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YATARAHISISHA UPATIKANAJI WA HAKI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora Mhe Haroun Ali Sleman amesema matumizi ya Teknolojia katika utowaji wa huduma za Msaada wa Kisheria kutarahisisha upatikanaji wa haki kwa Jamii kwa wakati.

SERIKALI KUIMARISHA SEKTA YA KILIMO

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuchukua juhudi katika kuimarisha Sekta ya Kilimo ili iweze kumsaidia Mkulima katika uzalishaji na upatikanaji wa uhakika wa Chakula Nchini na kuwa Endelevu.

Waziri wa Kilimo umwagiliaji Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis ameeleza hayo huko katika Bonde la Mpunga Kilombero wakati wa zoezi la Uzinduzi wa uvunaji wa Mpunga kwa Wakulima na Maafisa wa Kilimo.

MABADILIKO YA SHERIA KUIMARISHA UTENDAJI

Kamati ya kusimamia Ofisi za VIongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi imeshauri Serikali kuendelea kufanya tafiti kwa sheria mbali mbali ambazo zitatoa miongozo kwa Taasisi za umma ikiwa ni pamoja na kuimarisha suala la utowaji wa huduma

Akiwasilisha maoni ya Kamati hiyo kuhusiana na Mswada wa Sheria mbali mbali na kuweka masharti bora ndani yake Makamo mwenyekiti wa kamati hiyo Mh Maryam Thani juma amesema hatua hiyo itasaidia kukuza utendaji na utowaji huduma za uhakika

VIFO VYA MAMA NA MTOTO VYAFIKIA 20 KWA MWEZI JANUARI HADI MACHI

Waziri wa afya Mhe Nassor Ahmed Mazrui amesema kwa kipindi cha Januari hadi Machi Vifo vya Mama na Mtoto vilivyoripotiwa ni 20 kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo upungufu wa watoa huduma pamoja na ukosefu wa Vifaa Tiba bora katika Hospitali. 

Akizungumza katika makabidhisho ya Vifaa Tiba kupitia Programu ya Uzazi ni Maisha Wogging Mhe Mazrui amesema Serikali itaendelea na kuchukua juhudi mbali mbali ili kupunguza vifo hivyo.

ZAIDI YA KADI ELFU 44 ZIMETOLEWA NA ZEC

Jumla ya Kadi elfu 44  Mia Tano na 95 zimetolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa Watu waliojindikisha katika Daftari la kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza .

Akizungumza na Waandishi wa habari huko Maisara kuhusu ugawaji wa Kadi Mkurugenzi wa Uchaguzi Zanzibar Nd Thabit Idarous Faina amesema hatua hiyo imeonyesha kuwa Wananchi wana mwamko mkubwa  katika kuhakikisha wanatumia haki yao ya kupiga Kura wakati utakapofika na kwamba idadi hiyo.

RAIS WA ZANZIBAR DKT HUSSEIN ALI MWINYI ANAONGOZA KWA KUFUATA SHERIA NA KATIBA YA NCHI.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Charles Hilary amesema ,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi anaongoza kwa kufuata Sheria na katiba ya Nchi.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.