Habari

KAMBI ZA MATIBABU ZA MARADHI MBALIMBALI HUSAIDIA KUIMARISHA AFYA ZA WANANCHI

   Makamo wa Kwanza wa Rais Mhe.Othman Masoud Othman amesema Serikali imekuwa ikishirikiana na Wadau mbali mbali wa masuala ya Afya ili kuona kunapatikana huduma bora kwa Wananchi

    Akifungua Mkutano Mkuu wa Wataalamu wa Ugonjwa wa Macho Tanzania na Afrika Mashariki na Kati kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar amesema kupitia Mfumo wa Mashirikiano kati yao kumekuwa na ongezeko la Kambi za Matibabu ya Magonjwa mbali mbali na kuongezeka tafiti za Magonjwa yanayoathiri Jamii

MHE.HEMED AZITAKA TAASISI ZA SERIKALI KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
SMZ IMETENGA ENEO LA BANDARI JUMUISHI KUHAKIKISHA USALAMA WA UPOKEAJI NA UGAVI BIDHAA
SMZ KUIMARISHA HUDUMA YA MAJI KUPITIA WAHISANI

    Wizara ya Fedha na Mipango ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatarajia kupokea Euro Milioni 3 kutoka Taasisi ya Giz`3 ya Ujerumani zitakazo saidia kuimarisha upatikanaji wa huduma ya Maji Visiwani Zanzibar.

   Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wa (SMZ) Dkt.Juma Malik  wakati wa hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Makubaliano ya Mradi wa Maji na Taasisi ya Giz yaliyofanyika Jijini Dar-es -salaam.

NYUMBA ELFU TATU ZA BEI NAFUU ZATARAJIWA KUJENGWA KATIKA ENEO LA CHUMBUNI

   Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi imetiliana Saini na Kampuni ya Weihai Huatan kutoka China kwa lengo la Ujenzi wa Nyumba za Bei nafuu  ambazo zinatarajiwa kujengwa Eneo la Chumbuni Mkoa wa Mjini Magharibi.

   Akizungumza mara baada ya Utiaji Saini huko Naibu Waziri wa Wizara hiyo  Mhe Salha Mohammed Mwinjuma amesema hatua hiyo itasaidia kuondokana na matatizo ya upatikanaji wa Maakaazi kwa Wananchi ambapo Ujenzi wa Nyumba hizo umekusudia zaidi kwa Wananchi wa Kipato cha chini.

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WAHISANI KUKUZA KILIMO

     Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji Zanzibar Mhe.Shamata Shaame Khamis amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Wadau mbali mbali katika kukuza Sekta ya Kilimo kwa manufaa ya Wananchi na Taifa .

    Mhe.Shamata amesema hayo wakati alipokuwa akizundua Kituo cha Elimu ya Vitendo kwa Wakulima( Agro Connect ) huko Kangagani Pemba

    Mhe.Shamata amewataka Wakulima kukitumia Kituo hicho kwa kupata elimu ili waweze kubadili melekeo wa Kilimo na kulima

kilimo chenye tija huku wakipata chakula cha uhakika.

JESHI LA POLISI LAHIMIZWA KUONGEZA UFANISI KATIKA KAZI ZAO

    Kamishna wa Polisi Zanzibar  Hamad Khamis Hamad amewataka Watendaji wa Jeshi la Polisi sifa wanazozipata za ufanyaji kazi bora ziendane na huduma bora katika kuwatumikia Wananchi.

    Akikabidhi Nishani kwa  Wakaguzi na Askari 20 wa Vitengo vya Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,

   Kamishna  Hamad  amesema  ari ya uwajibikaji uende sambamba na kuondosha Kero za Wananchi wanapofuatilia haki zao kupitia vyombo vya sheria.

SERIKALI KUTUNGA KANUNI MPYA ZA UTOAJI LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI

   Serikali inatarajia Kutunga Kanuni Mpya za Utoaji Leseni za Uchimbaji wa Madini Nchini kuanzia Mwezi Julai Mwaka huu ili kuwadhibiti baadhi ya Watu wenye tabia ya kumiliki Leseni za Uchimbaji bila ya kuchimba na badala yake huzikodishwa kwa Wengine.

   Hali hiyo imeelezwa na Waziri wa Madini Nchini, Anthony Mavunde kwenye Mkutano wake na Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu katika Eneo la Ntambalale Kata ya Segese Wilaya Kahama Mkoani Shinyanga.

ZHELB YAZINDUA MFUMO WA UTOAJI MIKOPO MWAKA 2024/2025

   Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu Zanzibar imepanga kudhamini Wanafunzi zaidi ya Elfu 7 kwa Mwaka wa Masomo 2024/2025 ambapo kati yao Wanafunzi zaidi ya Elfu 4 wanaoendelea na Masomo na Wanafunzi Elfu 3 wanaoanza Masomo.

   Akizungumza katika Uzinduzi wa Muongozo wa Utowaji Mikopo na Mfumo wa Mikopo kwa Mwaka 2024/2025 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh.Ali Abdulghulama Hussein amesema hatua hiyo imesababisha kuongeza Bajeti ya Fedha kutoka Bilioni 29 Nukta 9 kwa Mwaka 2023 hadi Bilioni 33 Nukta 3 

JAMII INAHITAJI USAIDIZI WA KISHERIA KUTATUA MATATIZO YAO

   Kuwepo kwa Vituo vya Msaada wa kisheria ndani ya Vyuo Vikuu na Vituo  vinavyotoa huduma za sheria kutasaidia kukuza Elimu na kuwajengea moyo Watendaji  wanaotoa huduma hizo.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.