Habari

SMZ KUCHUKUA HATUA WANAOHARIBU MIKARAFUU

     Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema itawachukulia hatua za kisheria Wananchi watakaobainika kuharibu au kukata Mikarafuu kinyume na sheria. 

      Akizungumza na Wakulima na Wadau wa Karafuu kutathmini Msimu wa Karafuu uliopita huko Dunga Mkuu wa Wilaya ya Kati Sadifa Juma Khamis amesema vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya Wananchi vinaitia hasara Serikali.

WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KUTAKIWA KUENDELEZA MAMBO MEMA

    Waumini ya Dini ya Kiislam wametakiwa kuhimizana juu ya umuhimu wa kutunza amani na utulivu ili kuendelea kuishi katika mustakbali mwema.

    Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe.Hamza Hassan Juma katika Wiiki ya kuelekea kilele cha Mwaka Mpya wa Kiislam 1446 Hijria, 

    Amesema Uislam ni Dini iliyokuja kuondosha aina zote za Ubaguzi na ukandamizaji baina ya Watu, hivyo Waumini wa Dini ya Kiislam wanapaswa kujipambana na tabia njema ili kuepukana na matatizo yanayoweza kujitokeza.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWAASA VIJANA KUJIEPUSHA NA MATUMIZI NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amezindua Sera ya Taifa ya Dawa za Kulevya ya Mwaka 2024.

    Uzinduzi wa Sera hiyo umefanyika wakati wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani katika Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza. 

     Akizungumza katika Maadhimisho hayo, Waziri Mkuu amesema Tanzania sio mahali sahihi kwa biashara na Matumizi ya Dawa za Kulevya na ametoa wito kwa Vijana kuachana na Dawa za Kulevya zinazoathiri nguvu kazi ya Taifa.

WASTAAFU WA JESHI LA POLISI WATAKIWA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO

    Wastaafu wa Jeshi la Polisi wamesisitizwa kuendelea kutoa mchango wao katika suala zima la Ulinzi na Usalama katika ya Jamii ili kupunguza vitendo vya uhalifu vinavyoendelea Siku hadi Siku.

   Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa ametoa Wito huo katika Sherehe ya kuwaaga Wastaafu 50 wa Jeshi la Polisi waliokuwa wakifanya kazi katika Vituo mbali mbali vya Mkoa wake.

DC NGOLLO ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI WA KATA YA MKONGO MWINUKO NA MKONGO NAKAWALE

     Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Ngollo Malenya tarehe 27 Juni, 2024 amefanya mkutano wa hadhara wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata ya Mkongo mwinuko na Kijiji cha Mkongo Nakawale ambapo ameahidi kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hao.

WAHANDISI ZHC WATAKIWA KUONGEZA UMAKINI KATIKA MIRADI YA NYUMBA

    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar Ndg.Sultan Said Suleiman amewahimiza Wahandisi wa Shirika hilo kuongeza umakini katika kusimamia Miradi ya Ujenzi wa Nyumba ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati uliopangwa.

   Akizungumza katika Nyakati tofauti Wakati wa Ziara ya kutembelea Miradi ya ZHC na Maeneo ya Miradi mipya Ndg.Sultan amesema lengo la Ziara hiyo ni kuangalia na kufanya tathmini ya changamoto zilizopo katika Miradi hiyo ili kuendeleza juhudi za kuwapatia Wananchi Nyumba bora za Gharama nafuu.

WAZIRI MCHENGERWA AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Mhe.Mohamed Mchengerwa ,amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya  kusikiliza  Kero za Wananchi waliopo kwenye Vijiji, Mitaa na Vitongoji. 

    Waziri  Mchengerwa ametoa Maagizo hayo Jijini Dodoma Wakati Akizindua Programu ya uimarishaji wa Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

WADAU WA HABARI WATAKIWA KUZINGATIA MUONGOZO WA KURIPOTI MATUKIO YA UCHAGUZI

    Wadau wa Vyombo vya Habari  na Waandishi wa Habari wametakiwa kuzingatia maudhui ya Utangazaji na kufuata utaratibu wa miongozo ya kuripoti Habari  wakati wa Kipindi cha Uchaguzi.

    Akifungua Mkutano wa Wadau wa Vyombo vya Habari Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Utangazaji Zanzibar Suleiman Ame Khamis katika Kikao Maalum cha Maelekezo ya Wajibu wa Vyombo vya Habari kuzingatia maudhui na muongozo wakati wa Kuripoti Matukio ya Uchaguzi amesema ni vyema Waandishi Wahabari  kufuata Miongozo kama ilivyoekwa  wanapofanya  Kazi zao.

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA JAMHURI YA WATU WA CHINA

   Wizara ya Fedha na Mipango imesema itaendelea kushirikiana na Taasisi ya Dhamana na Mikopo kutoka Jamhuri ya Watu  wa China ili kuleta Maendeleo Nchini .

   Akizungumza na Ugeni huo kutokana China Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Sada Mkuya Salum amesema Zanzibar imekuwa na ushirikiano mzuri na Jamhuri ya Watu wa  China katika Sekta mbali mbali ikiwemo Michezo , Habari, Afya pamoja na kuwajengea uwezo Maafisa kwa kuwapatia Mafunzo mabali mbali.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.