Habari

TANZANIA NA MSUMBIJI KUANZISHA KITUO CHA PAMOJA CHA FORODHA

      Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Msumbiji zimekubaliana kuanzishwa kwa Kituo cha pamoja cha Forodha baina ya Mataifa hayo ili kuongeza fursa za Biashara.

     Hayo yameelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es salam wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Ziara ya Siku Tatu ya Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ambapo amesema bado mahusiano ya kibiashara baina ya Mataifa hayo yako chini.

MAENDELEO KATIKA SEKTA YA ANGA YATASAIDIA KUKUZA UCHUMI WA ZANZIBAR

    Kuimarika kwa Sekta ya Usafiri wa Anga kutachangia kuifungua Zanzibar Kiuchumi hasa katika Sekta ya Utalii.

    Akizundua Ndege ya Jambojet Q400 ambayo itaanza safari zake   kutoka Mombasa Kenya kuja Zanzibar katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi DkT.Khalid Salum Muhammed amesema hatua hiyo itachangia kukuza Uchumi hasa kwa Wafanyabiashara wadogo wadogo ambao wanatoa bidhaa zao Mombasa Kenya kwa kutegemea Majahazi. 

SMZ HAIJARIDHISHWA NA UJENZI WA SKULI YA SEKONDARI YA MAKUNDUCHI

    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali haijaridhishwa na kasi ya Ujenzi unaoendelea wa Skuli ya Sekondari ya Makunduchi jambo linalorejesha nyuma dhamira ya Dkt. Mwinyi ya kuhakikisha anaondoa matatizo zote kwa Wananchi ikiwemo Elimu kwa Wanafuzi wa Mikoa yote ya Zanzibar.

   Ameyasema hayo alipokagua Ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake ya kuitembelea Skuli hiyo kila Mwezi.

SMZ YAZIDI KUJIPNGA KATIKA KUWAPATIA WANANCHI WAKE MAENDELEO

    Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikichukua mbalimbali kutafuta Wawekezaji ili kuona inawapatia Maendeleo Wananchi wake. 

    Akizungumza mara baada ya kutembelea Mradi wa Kuku Mama Kizimbani Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Mali asili na Mifugo    Mhe. Shamata Shame Khamis amesema Mradi huo ambao chini ya Mwekezaji kutoka China utaweza kuwa Mkombozi kwa Wazanzibar katika upatikanaji wa Ajira na kuwasaidia kuendeleza ufugaji pamoja na kutafutiwa Soko.

SHIRIKA LA WORLD VISION TANZANIA LIMEKABIDHI MIRADI WILAYA YA KILOSA

   Halmashauri Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro imekabidhiwa Miradi ya Maendeleo iliyopo Tarafa ya Ulaya kutoka Shirika la World Vision Tanzania ikiwemo Miradi ya Visima vya Maji vinavyotumia Nishati ya jua, Vituo vya Afya na Mradi wa Skuli ya Msingi Madudumizi, itakayowanufaisha zaidi ya Wananchi Elfu Kumi wa Eneo hilo.

ZANZIBAR KUFANIKISHA UPASUAJI WA MIDOMO WAZI

    Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui amesema kwa sasa Zanzibar imefanikiwa kuwafanyia upasuaji Watoto na Watu Wazima wenye Midomo wazi kwa awamu tofauti.

    Amesema katika hatua hiyo iliyofikiwa Wizara itaendelea kushirikiana na Taasisi mbali mbali hasa The same Qualities katika kuimarisha afya za wenye matatizo ya Midomo wazi kwa kuwapatia matibabu kupitia Wataalamu hao na wanaotoka Nje ya Nchi.

JAMII YA MASASI MKOANI MTWARA WADUMISHA MILA NA DESTURI ZA UNYAGO

    Wakazi wa jamii ya Masasi Mkoani Mtwara wadumisha Mila na desturi za unyago wa kimila

     Wakazi wa kijji cha Nangoo wamekiri kudumisha Mila zao Kila ifikapo mwezi wa 6 na mwezi wa 12 na kwa watoto waliofikia umri wa miaka 7 mpaka 10 wakike na kiume upelekwa porini kupata mafunzo ya kimila yenye lengo la kuwafanya watoto kua na heshima,  kujituma, nidhamu pia kufanya vizuri katika kazi mbali mbali.

     Ndugu Venant Isaya Gabriel Mwenyekiti wa kijji cha Nangoo amekiri kutokea kwa mila hizo maarufu unyago katika miezi hio

DKT.MWINYI AWATAKA WANASIASA KUSHINDANA KATIKA KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewataka wanasiasa kushindana kuwaletea wananchi huduma bora za kijamii kimaendeleo.

    Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa kama yeye amejenga hospitali kila Wilaya na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii iwe ni mashindano na siyo kuleta hoja za uvunjifu wa amani.

     Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo wakati wa makabadhiano na ufunguzi nyumba za Wafanyakazi wa Hospitali ya Abdullah Mzee , Mkoa wa Kusini Pemba .

TAMWA YAWAHIMIZA WANAWAKE KUSHIRIKI KATIKA MICHEZO

    Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA-Zanzibar) kimesema ni wajibu kwa Wanawake  kushiriki Michezo kutokana na kuimarisha Afya zao na kupata fursa ya Ajira.

    Akizungumza katika madhimisho ya Siku ya  Mtoto wa Afrika Mkurugenzi wa Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA-Zanzibar) Dkt. Mzuri Issa amesema asilimia kubwa ya Wanawake bado wako nyuma katika kushiriki Michezo jambo ambalo limesababisha kuwa nyuma kimaendeleo na kushindwa kufikia ndoto zao.

WANANCHI WA KIJIJI CHA UZI WATAKIWA KUTOA MASHIRIKIANO KWA POLISI JAMII

   Mkuu wa Wilaya ya Sadifa Juma Khamis , amewataka Wananchi wa Kijiji cha Uzi kutoa ushirikiano wa dhati na Askari Jamii wa Shehia hiyo ili Kisiwa hicho kiendelee kubaki salama pamoja na Wakaazi wake.

    Amesema hayo huko katika Kijiji cha Uzi, katika Sherehe ya kuwapongeza Askari Jamii kwa kazi  ya kupunguza Vitendo viovu vikiwemo vya Wizi, amesema ni hatua nzuri iliyofikiwa kwa sasa, hivyo amewasisitiza Askari hao kutochoka kuwakabili wale wanaorudia au kujaribu kufanya vitendo visivyo halali.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.