Wawekezaji wa Kampuni ya Sumsang inayoshughulikia Ujenzi na Viwanda kutoka Jamhuri ya Watu wa Korea wameelezea kuvutiwa na fursa za uwekezaji zinazopatikana Zanzibar.
Kiongozi wa ujumbe huo wa Wawekezaji, Yonyi Yi, katika mazungumzo na Watendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar ZIPA huko Maruhubi na Wadau wa Uwekezaji, amesema wamejionea maeneo ambayo ni Kivutio kwa kuanzisha Miradi mbali mbali ya Kiuchumi.
Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Watu wa Korea, Balozi Togolani Edriss Mavura, amesema Kampuni hiyo kubwa katika Miradi mbali mbali imekuja Tanzania ikiwa ni Mpango wake wa kuanzisha Miradi katika Bara la Afrika na kuonesha kuvutiwa na Ujenzi wa Bandari ya Mangapwani.
Akizungumza kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA, Mkurugenzi Masoko na uwenezi Emanuel Mashimba, amesema Serikali imekuwa ikiimarisha Miundombinu ya usafiri na Mawasiliano pamoja na kufanya Mikutano na Wafanyabiashara wa Kimataifa kama sehemu ya kuitangaza Zanzibar.
Nao Wadau wa masuala ya uwekezaji kupitia Taasisi mbali mbali wamesema kuwa uwekezaji uliopo Nchini umekuwa ni sehemu ya kuongezeka pato la Taifa.