Kamati ya Siasa ya Jimbo la Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, imefanya Ziara katika miradi ya kimkakati katika Jimbo hilo ili kuuangalia maendeleo na matatizo yanayojitokeza katika miradi hiyo.
Kamati hiyo ikiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Micheweni Mh.Abdi Hijja Mkasha pamoja na mwakilishi wa jimbo hilo Mh. Shamata Shaame Khamis
Akizungumza baada ya Ziara hiyo Mbunge wa Jimbo hilo Mhe.Abdi amesema kamati hiyo itaendelea kufuatia hatua kwa hatua miradi hiyo ili kuhakikisha inakamilika kwa muda uliotakiwa.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Wadi ya Micheweni Ndg. Ali Haji Mbwana na Katibu wa Wadi ya Kiuyu Maziwa Ng’ombe Ndg. Juma Sefu Juma wameipongeza Serikali ya awamu ya nane kwa kuwaletea miradi ya maendeleo kwenye Jimbo hilo.
Katika ziara hiyo kamati ya sisasa ilitembelea tofauti kwenye Jimbo hilo ikiwemo ujenzi wa bara bara ya Michweni Mziwangombe ujenzi wa bandari ya Shumba ya Mjini pamoja na Hospitali ya Wilaya hiyo.