JUMUIYA YA MUZDALIFA IMESHAURI TAASISI ZA KIJAMII KUSHIRIKIANA

KATIBU MKUU JUMUIYA YA MUZIDALFA

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Muzdalifa Farouk Hamad amesema ameshauri Taasisi za Kijamii kushirikiana na kuwa na malengo ya pamoja katika kuifikia Jamii.

Akikabidhi Msaada wa vitu mbambi mbali kwa Masheha na Yatima katibu Farouk amesema malengo ya pamoja yataisaidia Serikali katika kukuza ustawi wa Jamii

Amesema hayo wakati akikabidhi Msaada huo  na kuipongeza Serikali kwa kuendelea kuwapunguzia ushuru katika mambo yanayohusu Jamii.

Afisa Zaka na Misaada Shehe  Dau Silima Ali amesema kuwa kuisaidia jamii kunarahisisha na kupunguza ugumu wa Maisha  Watu wanaoishi katika mazingira magumu.

Amesema Serikali itaendelea kuzingatia njia bora zaidi za kuendelea kupunguza gharama katika kuwapatia huduma Wananchi wake.

Sheha wa Shehiya ya Mkele akitoa shukrani baada ya Wananchi kupata Msaada huo  ameziomba Taasisi nyengine kuiga mfano huo na kutoa kwa ajili ya Allah.

Msaada uliotolewa ni Maboksi ya nguo, Viatu na Vifaa vya Skuli  kwa Wanafunzi wa Skuli ya Nyerere Sekondari.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.