Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amewataka Watendaji wa Jeshi la Polisi sifa wanazozipata za ufanyaji kazi bora ziendane na huduma bora katika kuwatumikia Wananchi.
Akikabidhi Nishani kwa Wakaguzi na Askari 20 wa Vitengo vya Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,
Kamishna Hamad amesema ari ya uwajibikaji uende sambamba na kuondosha Kero za Wananchi wanapofuatilia haki zao kupitia vyombo vya sheria.
Kamishna msaididi Mwandamizi wa Polisi Ngoi amesema Nishani na Zawadi wanazopewa Askari wa Jeshi la Polisi itakuwa ni chachu ya kufanya kazi kwa kuzingatia haki, weledi, uaminifu na nidhamu
stories
standard