Kuwepo kwa Vituo vya Msaada wa kisheria ndani ya Vyuo Vikuu na Vituo vinavyotoa huduma za sheria kutasaidia kukuza Elimu na kuwajengea moyo Watendaji wanaotoa huduma hizo.
Akifungua Kongamano la masuala ya msaada wa kisheria kwa Wanafunzi hao Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim amesema Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora kwa kushirikiana na Shirika la Legal Service Facility na Undp imeandaa Muongozo wa Uanzishwaji wa Vituo hivyo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma bora na kuondoa Migogoro ndani ya Jamii.
Mashauri wa Program za Utawala Bora kutoka Shirika la Undp Godfrey Mulisa amesema Shirika hilo litashirikiana na Serikali kuhakikisha Elimu ya msaada wa kisheria inaendelea kutolewa ili kuwawezesha wasio na uwezo kupata haki zao.
Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na msaada wa kisheria Hanifa Ramdhan Said na Kaimu wa Kitivo cha Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar University Dokta Sikujuwa Omar Hamdani lengo ni kuielimisha Jamii juu ya masuala mbali mbali ya Msaada wa Kisheria.
Jumla ya Mada Tatu ziliwasilishwa katika Kongamano hilo ikiwemo athari za Dawa za Kulevya kwa Vijana, Sheria za usafirishaji haramu wa Binadamu na dhana ya huduma ya msaada wa kisheria