DKT.WMINYI AWATAKA VIONGOZI KUFANYA KAZI KWA BIDII

Uapisho wa Mwaziri

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Viongozi kufanya kazi ya kuwatumikia Wananchi kwa mujibu wa sheria.

     Akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi aliowateuwa hivi karibuni huko katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar Dkt Mwinyi amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza fursa hasa katika sekta muhimu kwa uchumi ikiwemo sekta ya utalii.

    Akizungumzia suala la kujiuzulu kwa Mawaziri Dkt. Mwinyi amesema kuwa ni jambo la kawaida hata hivyo amewataka Mawaziri hao kuwajibika panapo stahiki na kusema ukweli sambamba na kuwaagiza Watendaji wa Wizara ya ardhi kuhakikisha wanatatua migororo ya ardhi kwa ushirikiano.

     Nao Mawaziri waliokula viapo kwa upande wao wameeeleza vipaumbele vyao na azma katika kutekeleza majukumu yao.

      Walioapishwa katika hafla hiyo ni pamoja na Mhe. Shaaban Ali Othman Waziri wa uchumi wa buluu na uvuvi na Mhe. Waziri wa utalii na mabo ya kale Mhe.  Mudriq Ramadhan Soraga na Viongozi wengine.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.