Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar ina miradi mingi inayohitaji Wawekezaji kuja kuwekeza.
Katika mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara na Reli CCECC kutoka China amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo tayari kushirikiana na Kampuni hiyo kutimiza ndoto ya kuijenga upya Zanzibar.
Aidha Dkt.Mwinyi ameitaka Kampuni hiyo kufikiria kuanzisha Kiwanda cha Dawa za kutibu Binadamu Zanzibar kutokana na pia kujihusisha na Sekta hiyo muhimu huku akiiomba kuingia katika Sekta ya Utalii ikiwa ni Sekta Mama kwa Uchumi wa Zanzibar.
Uongozi wa Kampuni ya CCECC iliyojenga Reli ya Uhuru-Tazara Mwaka 1970 ya Tanzania na Zambia, imeonesha kuvutiwa kushiriki kujenga Reli Zanzibar ikiwa ni azma ya Dkt .Mwinyi kwa Zanzibar kuwa na Usafiri huo
Wakati huo huo Dkt.Mwinyi amewakaribisha Wawekezaji kutoka Korea kuja kuwekeza Zanzibar katika Sekta mbalimbali ikiwemo Uchumi wa Buluu, Ujenzi wa Kumbi za Mikutano ya Kimataifa.
Katika Mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Kudumu ya Bunge la Korea, Sul Hon na Ujumbe wake ameishukuru Serikali ya Korea kwa kuendelea kuisaidia Zanzibar katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya Sekta ya Elimu, Afya na Uvuvi.