DKT. SAMIA KUTARAJIWA KUFANYA ZIARA NCHINI INDONESIA

WAZIRI WA MAMBO YA NJE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya Kitaifa Nchini Indonesia kwa lengo la kukuza na kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia na kuimarisha uhusiano wa Kiuchumi kati ya Nchi hizo mbili kupitia Sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Nishati, Madini, Elimu, Uchumi wa Buluu na ulinzi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa mambo ya Nje Mheshimiwa January Makamba alipokua akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa Tanzania na Indonesia zina uhusiano wa muda mrefu wa Kihistoria ambao umetimiza Miaka 60 ikinufaika kwa kuuza Bidhaa mbalimbali ikiwemo mbegu za Mafuta, Matunda, Kahawa, Chai, Pamba na Tumbaku.

Amesema mbali na ziara hii ya Indonesia inayotarajiwa kufanyika tarehe 24 hadi  26 January 2024 Mheshimiwa Rais Dk Samia Suluhu Hasaan pia anatarajiwa kufanya ziara ya Kitaifa Nchini Vatican Tarehe 11-12 Feruary 2024 kufuatia mwaliko wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Fransi na Tarehe 13-14 February 2024 atafanya Ziara ya Kitaifa Nchini Norway.

Mbali na ziara hizo Tanzania nayo katika kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia na Nchi na Mashirika ya Kimataifa ili kukuza maendeleo ya Uchumi, Biashara, Uwekezaji na ushirikiano katika Sekta mbalimbali inatarajia kupokea Viongozi wa Tatu kutoka Nchini China, Cuba na Poland katika kipindi hiki cha January hadi February 2024.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.