Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Ngollo Malenya tarehe 27 Juni, 2024 amefanya mkutano wa hadhara wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata ya Mkongo mwinuko na Kijiji cha Mkongo Nakawale ambapo ameahidi kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hao.
Katika mkutano huo DC Malenya aliambatana Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkurugenzi Pamoja na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo na wengine kutoka Taasisi zinazowahudumia wananchi kwa ukaribu ikiwemo Wakala wa Barabara za Vijijini na Mji (TARURA) , Wataalamu kutoka Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) pamoja na wataalamu kutoka Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO)pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Akiwa katika kusikiliza kero za wananchi wa Kata ya Mkongo Mwinuko , DC Ngollo Malenya amepokea changamoto mbalimbali zikiwemo za Elimu, Miundombinu ya barabara, Maji, Umeme, Afya, migogoro mbalimbali ya Ardhi na changamoto za Kisheria ambapo zipo alizotatua papo kwa papo na nyingine kuzipatia utatuzi kwa kuwataka watendaji kuhakikisha wanazishughulikia Mara moja.
Hatahivyo, DC Malenya amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Kwa Kutenga Fedha nyingi kwaajili ya Kuboresha Miundombinu mbalimbali ikiwemo Miundombinu ya Maji,Barabara Shule,Afya,Umeme na Miundombinu mingine Ambayo inawasaidia Wananchi wa Wilaya ya Namtumbo kupata Huduma Mbalimbali za Kijamii.