CHINA NA ZANZIBAR KUONGEZA WIGO KATIKA FANI ZA BAHARI

UTIAJI SAINI

       Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar na Wizara ya Maliasili ya Jamuhuri ya Watu wa China zimetilian saini hati ya mashirikiano na bahari ya Jamuhuri ya Watu wa China ili kuendeleza vyema sera ya Uchumi wa Buluu.

       Waziri wa fedha na mipango Zanzibar Dkt. Saada Mkuya Salum amesema hayo kwa niaba ya Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe .Shaabani Ali Othman huko Maisara amesema Zanzibar ina fursa nyingi za kutekeleza ajenda ya uchumi wa buluu hivyo amewataka Wananchi kutumia fursa hiyo

      Dk. Saada amesema ushirikiano huo Unakwenda kuongeza uhifadhi wa mazingira ya bahari na kueleza kuwa Zanzibar teknolojia katika masuala ya bahari huku akisema Vijana watakaosomea fani hizo za bahari wataongeza wigo kati ya China na Zanzibar.

      Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Dkt. Aboud Suleiman Jumbe amesema China ina fursa nafasi za Elimu kwa Wanafunzi wanaotoka Zanzibar kujiunga na fani za bahari ikiwemo ufugaji wa samaki na majongoo hivyo amewataka Vijana wanapomaliza kusoma kwenda kujiunga na fani hizo ili kujiajiri.

      Naibu Waziri wa Maliasili wa China Mhe. Sun Shuxian amesema wataendelea kushirikiana na Zanzibar katika masuala ya bahari na kuendeleza Sekta hiyo kwa maslahi ya nchi hizo mbili.

standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.