Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imeandaa Mkutano wa Kimataifa utakaoambatana na Mafunzo Maalum ya Matibabu ya Moyo ili kuongeza Utaalamu utakaoimarisha zaidi huduma za matibabu
Akitoa taarifa Mkurugenzi Mtendaji Taasisi hiyo Dkt Peter Kisenge Amesema Mkutano huo utashirikisha Wataalamu wa Mataifa 40 wakiwemo Madaktari Bingwa una lengo la kuitangazaTanzania kuwa kimbilio la Matibabu ya Moyo
Amesema Ugonjwa wa Moyo ukiwa ni miongoni mwa Magonjwa matatu yanayoongoza kwa Asilimia 25 umesababisha Serikali kuwekeza Wastani wa Shilingi Bilioni 60 kwa ununuzi wa Vifaa na kuiwezesha Taasisi hiyo kuokoa Asilimia 90 ya Wagonjwa kusafirishwa kwa ajili ya Matibabu
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo Dkt .Asha Ressa Zinna amewaomba Wananchi watumia fursa ya kufuatilia Mkutano huo ili kujitambua endapo wana dalili za tatizo la moyo
Mratibu wa Mkutano huo Dk Godwin Sharaw amesema kupitia Mkutano huo wataweza kujadili vikwazo na kupeana uzowefu hasa katika njia za kisasa za upasuaji
Mkutano huo utawashirikisha Wataalamu zaidi ya Mia tano wa Mataifa tofauti yakiwemo Egypt,Marekani na Uturuki unatarajiwa kufunguliwa kesho na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dk Philip Mpango