Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Bembela Ndg.Ramla Moh'd Ramadhan amesema kuwa Skuli ya Benbela imefanya vyema tokea kuanzishwa kwake Miaka mia na haijawahi kutetereka.
Akizungumzia tamasha la kuadhimisha Miaka mia moja ya mafanikio tokea kuanzishwa kwa Skuli hiyo Ndg.Ramla amesema kuwa katika mikondo tofauti iliyopitia Skuli hiyo bado inaendeleza ubora wake kwa kutoa vipaji.
Amesema February 18 Mwaka huu Skuli hiyo inakusudia kufanya Tamasha kubwa litakalowakutanisha Wwadau na Wasomi waliosoma Skuli hiyo.
Mwenyekiti huyo amesema kabla ya Tamasha hilo litatanguliwa na wiki ya Benbela ambayo itakuwa na maonesho na mMidahalo na kuwasilisha maendeleo ya Skuli.
Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Elimu amesema tayari Wizara imeshatoa baraka ya utekelezaji wa Tamasha hilo.
nao Wajumbe wa kamati ya maandalizi wamesema wameanza kuwashirikisha Wadau ili Tamasha la karne liweze kuwa na faida