WAANDISHI WA HABARI WAMETAKIWA KUTUMIA VIZURI TAALUMA ZAO

Waandishi wa habari

     Waandishi wa Habari wametakiwa kutumia vizuri Teknolojia ya Habari ili kuihabarisha Jamii kuhusu takwimu za Sensa ya Watu na makaazi ya Mwaka 2022 na kuwepo matumizi sahihi ya Takwimu hizo.

     Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Ndg. Beno Malisa, wakati akifungua Semina kwa Waandishi wa Habari wa Mikoa ya Mbeya, Iringa na Songwe kuhusu usambazaji na uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.

      Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 Tanzania Bara Ndg.Anne Makinda, amesema kazi ya Sensa ina awamu tatu, awamu ya kwanza ilikuwa kuhamasisha Wananchi wajitokeze kushiriki kujiandikisha, Awamu ya Pili ilikuwa Siku ya kuhesabu ambapo Watu walijitokeza kwa wingi na sasa ni Awamu ya Tatu na kwamba Awamu zote hizo ni Vyombo vya Habari vimefanya kazi kubwa.

    Akizungumza kwa niaba yaWaandishi wa Habari Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya Ndg.Nebart Msokwa, ameishukuru Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kuona kuwa Waandishi wa Habari ni Wadau muhimu katika kuhamasisha matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na makazi ya Mwaka 2022.

hot
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.