Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mwinyi meyasema hayo katika muendelezo wa shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Mwinyi ameweka jiwe la msingi ujenzi wa Soko la kisasa Mwanakwerekewe ambapo amezitaka mamlaka husika kuhakikisha kuwa licha ya maombi mapya ya wafanyabiashara katika soko hilo, wahakikishe wafanyabiashara waliopisha ujenzi wanazingatiwa.
Aidha Rais Mwinyi amesisitiza dhamira ya Serikai kuhakikisha malengo iliyoyaweka yanatekelezwa huku akiwasisitiza wananchi kupuuza kauli zenye nia ya kupotosha malengo hayo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Masoud Ali Mohamed amesema ni wajibu wa kila Mtu kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo.
Akitoa taarifa ya kitaalamu ujenzi wa Soko hilo, Katibu Mkùu Tamisemi Issa Mahfoudh Haji, amesema ujenzi wa Soko hilo lenye ghorofa mbili utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 35.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib,Idrisa Kitwana Mustafa amepongeza juhudi za Serikali kwa kutimiza ahadi zake.